Benki ya NBC Yazidua Akaunti ya Mfugaji Mahususi kwa Wadau wa Sekta ya Ufugaji.

 Benki
ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua ‘Akaunti ya Mfugaji’ mahususi kwa
ajili ya wadau wa sekta ya ufugaji nchini wakiwemo wafugaji,
wanenepeshaji mifugo, wafanyabiashara wa mifugo, wasafirishaji wa mifugo
mifugo na wadau mbalimbali wanaohudumia sekta hiyo muhimu kiuchumi.


Huduma
hiyo ya kwanza kutambulishwa na benki ya biashara nchini maalumu kwa
kundi hilo, pamoja na kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta hiyo kupitia
huduma za fedha zilizorahisishwa zaidi pia inalenga kuunga mkono
jitihada za serikali katika kuandaa uchumi jumuishi kwa makundi yote ya
uzalishaji kupitia huduma bora za kifedha.

Hafla ya utambulisho
wa huduma hiyo kitaifa imefanyika leo kwenye soko la mnada wa mifugo la
Pugu lililopo wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, ikiongozwa na Mkuu
wa wilaya hiyo (DC), Edward Mpogolo sambamba na viongozi wengine
waandamizi wa wilaya hiyo, wadau wa biashara ya mifugo wakiwemo
viongozi na wafanyabiashara wa soko hilo. Mkurugenzi wa Idara ya wateja
wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC Elibariki Masuke aliwaongoza maofisa
wengine wa benki hiyo kwenye uzinduzi huo.

Akizungumza kwenye
hafla hiyo, DC Mpogolo pamoja na kuipongeza benki ya NBC kwa kubuni
huduma hiyo muhimu, alisema ujio wa huduma hiyo ni ukombozi mkubwa kwa
wadau wa sekta ya mifugo nchini kutokana na uwepo wa changamoto ya
ukosefu wa huduma za kibenki zinazoendana na mahitaji maalum ya kundi
hilo hali ambayo imekuwa ikisababisha wengi wao kuamua kutumia huduma za
kifedha zisizo rasmi na hivyo kuhatarisha usalama wao na fedha zao.

“Kwa
mfano katika mnada huu wa Pugu unahusisha mzunguko wa fedha wastani wa
kiasi cha Tsh bilioni 1 kila siku huku wengi wa wafanyabiashara
wakilazimika kutembea na fedha taslimu kitu ambacho ni hatarishi kwao
binafsi na mitaji yao. Hivyo ujio wa huduma hii ya Akaunti ya Mfugaji
iliyobuniwa kwa ajili yao utakuwa suluhisho la changamoto hii kwasababu
huduma za kifedha ikiwemo miamala zitapatikana kwenye maeneo ya minada
hii karibu yao kabisa,’’ alisema.

Hata hivyo Mpogolo aliiomba
benki hiyo kupitia huduma hiyo kuhakikisha inawasaidia zaidi wafugaji
kwa kuwekeza zaidi kwenye suala zima la utoaji wa elimu ya fedha, elimu
kuhusu ufugaji wa kisasa na elimu ya masoko ili wafugaji wawaweze
kunufaika zaidi na idadi kubwa ya mifugo waliyonayo kupitia ufugaji na
uwekezaji wa kisasa kwenye sekta hiyo.

Awali akiizungumzia
huduma hiyo, Masuke alisema inahusisha wafugaji mmoja mmoja na vikundi
huku ikitoa faida mbalimbali kwa wafugaji hao ikiwemo mikopo mbalimbali
kwa waufugaji na biashara wa sekta hiyo huku ikiwa haiusishi makato ya
uendeshaji wa akaunti kila mwezi, kupata taarifa za akaunti bila makato,
gharama nafuu za utoaji wa fedha, huduma za kibenki kwa njia ya simu
(NBC Kiganjani) huku muhusika akinufaika na nyongeza ya asilimia 2
kwenye akiba yake kila mwezi.

“Kwa upande wa wafugaji wa vikundi
au vyama pia hawatakiwi kuwa na hofu sababu watakuwa na uhuru wa kuweka
na kutoa fedha zao wakati wowote na pia watapata kitabu cha hundi kwa
gharama nafuu wachotakiwa ni kufungua akaunti bure kabisa kwenye matawi
yeto kote nchini,’’. Alisema.

Akifafanua zaidi kuhusu huduma
hiyo Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka
Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa alisema inahusisha wafugaji wa mifugo
ya aina zote wakiwemo ng’ombe na kuku na hatua hiyo ni mwendelezo wa
jitihada za benki hiyo kuyafikia makundi yote ya uzalishaji kufuatia
uzinduzi wa huduma kadhaa za mahususi kwa wakulima ikiwemo bima ya afya.

“Ni karibuni tu tumetoka kuzindua huduma ya Bima kwa wakulima
nchini nzima sambamba na sasa ni wakati muafaka pia kuwageukia wafugaji
nao waweze kunufaika na huduma hizi za NBC mahususi kwao ikiwemo huduma
hiyo ya bima,’’ alisema.

Wakizungumzia huduma hiyo, Mkuu wa
Mnada wa Pugu, Noel Byamungu na Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa mifugo
kwenye mnada huo, Iddy Maziku walisema imekuja wakati muafaka na itakuwa
suluhisho kwa wafugaji, wafanyabiashara wa mifugo na wadau wengine
sokoni hapo ambao kwasasa baadhi yao wanalazimika kutembea na kiasi
kikubwa cha fedha taslimu kwenye mifuko kutokana na kutokuwepo kwa
huduma za kifedha zinazoendana na mahitaji yao karibu na maeneo ya
minada hiyo.

“Ujio wa huduma hii utatusaidia kwa kiasi kikubwa
sisi wadau wa sekta hii ya mifugo. Inawezekana tayari tunahudumiwa na
taasisi za nyingine za kifedha zikiwemo zile ambazo sio rasmi lakini
ujio wa huduma hii mahususi kwa ajili yetu itakuwa ni suluhisho na
kambilio kwetu. Tunaamini kupitia huduma hii sasa hatulazimika tena
kutembea fedha taslimu ili kufanya malipo ya manunuzi ya mifugo na
huduma nyingine. Uzuri zaidi huduma hizi sasa zitakuwa zinatufuata
mahali tulipo na hivyo kutuhakikishia usalama wetu na fedha zetu…kwa
hili tunawashukuru sana NBC,’’ alisema Maziku.

Mkuu wa wilaya ya Ilala,
Edward Mpogolo (wa nne kulia)maoifisa wa benki ya NBC akiwemo  sambamba na wadau wengine wa sekta ya mifugo
wakiwemo
Mkurugenzi
wa Idara ya wateja wadogo na Wakubwa wa
benki ya NBC Elibariki Masuke (wa tatu), Mkuu wa Idara ya Masoko ya
benki hiyo
David Raymond (wa sita kulia) pamoja na wadau wa biashara ya mifugo
wakimsiliza
 Mkuu wa Mnada wa mifugo kwenye soko la
mifugo la Pugu, Noel Byamungu akielezea kuhusu hali ya biashara kwenye
 mnada huo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa   ‘Akaunti ya Mfugaji’
 ya benki ya NBC mahususi kwa ajili ya wadau wa
sekta ya ufugaji nchini. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki
kwenye mnada
huo.

Mkuu wa wilaya ya
Ilala, Edward Mpogolo (alievaa suti) sambamba na maoifisa wa benki ya NBC
akiwemo  Mkurugenzi wa Idara ya wateja
wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC Elibariki Masuke (katikati alievaa kofia) sambamba
na wadau mbalimbali wa sekta ya mifugo wakiwemo wafanyabishara  wa mifugo wakionyesha huduma mbalimbali
zinazopatikana kupitia ‘Akaunti ya Mfugaji’ 
ya benki ya NBC wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa  akaunti hiyo  mahususi kwa ajili ya wadau wa sekta ya
ufugaji nchini. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye mnada wa mifugo
wa Pugu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye
hafla hiyo, DC Mpogolo  pamoja na
kuipongeza benki ya NBC kwa kubuni huduma hiyo muhimu, alisema ujio wa huduma
hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wadau wa sekta ya mifugo nchini kutokana na uwepo
wa changamoto ya ukosefu wa huduma za kibenki zinazoendana na mahitaji maalum
ya kundi  hilo hali ambayo imekuwa
ikisababisha wengi wao kuamua kutumia huduma za kifedha zisizo rasmi na hivyo
kuhatarisha usalama wao na fedha zao.

Awali akiizungumzia
huduma hiyo, Masuke (pichani) alisema inahusisha wafugaji mmoja mmoja na
vikundi huku ikitoa faida mbalimbali kwa wafugaji hao ikiwemo mikopo mbalimbali
kwa waufugaji na biashara wa sekta hiyo huku ikiwa haiusishi  makato ya uendeshaji wa akaunti kila mwezi,
kupata taarifa za akaunti bila makato, gharama nafuu za utoaji wa fedha, huduma
za kibenki kwa njia ya simu (NBC Kiganjani) huku muhusika akinufaika na
nyongeza ya asilimia 2  kwenye akiba yake
kila mwezi.

Akifafanua zaidi
kuhusu huduma hiyo Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima
kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (pichani) alisema inahusisha wafugaji wa
mifugo ya aina  zote wakiwemo ng’ombe na
kuku na hatua hiyo ni mwendelezo wa jitihada za benki hiyo kuyafikia makundi
yote ya uzalishaji kufuatia uzinduzi wa huduma kadhaa za mahususi kwa wakulima
ikiwemo bima ya afya.

Akizungumzia huduma
hiyo, Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa mifugo kwenye mnada huo, Iddy Maziku  (Pichani) alisema imekuja wakati muafaka na
itakuwa suluhisho kwa wafugaji, wafanyabiashara wa mifugo na wadau wengine
sokoni hapo ambao kwasasa  baadhi yao
wanalazimika kutembea na kiasi kikubwa cha fedha taslimu kwenye mifuko kutokana
na kutokuwepo kwa huduma za kifedha zinazoendana na mahitaji yao karibu na
maeneo ya minada hiyo.

Mwenyekiti wa
wafanyabiashara wa mifugo kwenye mnada wa Pugu, Iddy Maziku  (kushoto) akifungua akaunti ya mfugaji ya
benki ya NBC wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa  akaunti hiyo 
mahususi kwa ajili ya wadau wa sekta ya ufugaji nchini. Uzinduzi huo
ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye mnada wa mifugo wa Pugu jijini Dar es
Salaam.

Baadhi ya wadau wa sekta
ya mifugo wakiwemo wafanyabishara wa mifugo wakifuatilia uzinduzi wa akaunti ya
mfugajiya benki ya NBC wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa  akaunti hiyo 
mahususi kwa ajili ya wadau wa sekta ya ufugaji nchini. Uzinduzi huo
ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye mnada wa mifugo wa Pugu jijini Dar es
Salaam

Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (alievaa
suti) akimpongeza Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya
NBC Elibariki Masuke kwa ujio wa  ‘Akaunti
ya Mfugaji’  ya benki ya NBC mahususi kwa
ajili ya wadau wa sekta ya ufugaji nchini. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa
wiki kwenye mnada wa mifugo wa Pugu jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya
Masoko wa benki ya NBC David Raymond akionyesha huduma mbalimbali
zinazopatikana kupitia ‘Akaunti ya Mfugaji’ 
ya benki ya NBC wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa  akaunti hiyo 
mahususi kwa ajili ya wadau wa sekta ya ufugaji nchini. Uzinduzi huo
ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye mnada wa mifugo wa Pugu jijini Dar es
Salaam.

Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (alievaa
suti) sambamba na maoifisa wa benki ya NBC akiwemo  Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na
Wakubwa wa benki ya NBC Elibariki Masuke (katikati alievaa kofia) sambamba na
wadau mbalimbali wa sekta ya mifugo wakiwemo wafanyabishara  wa mifugo wakionyesha huduma mbalimbali
zinazopatikana kupitia ‘Akaunti ya Mfugaji’ 
ya benki ya NBC wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa  akaunti hiyo 
mahususi kwa ajili ya wadau wa sekta ya ufugaji nchini. Uzinduzi huo
ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye mnada wa mifugo wa Pugu jijini Dar es
Salaam.

 

Related Posts