Compact Energies yashinda tuzo ya huduma bora Afrika

Kampuni ya Compact Energies Limited inayohusika na uzalishaji wa umeme Jua imeshinda tuzo ya makampuni makubwa barani Afrika katika utoaji wa huduma wa sekta ya Nishati katika vipengele vitatu vya, Uhandisi, Manunuzi na Matengeneyo ya Umeme Jua (Engineering, Procurement and Construction Solar Energy Company of the year 2024 in Large Size Category).

Tuzo hizo zinazojulikana kama ACOYA ( Africa Company of the Year Awards), zimetolewa usiku wa Mei 31,2023 katika ukumbi wa the Super Dome Masaki, jijini Dar es Salaam na kushindanisha zaidi ya makampuni 700 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, ambapo kati ya kampuni hizo, 134 zilifanikiwa kupita katika mchujo wa tathmini.

Hii ni tuzo ya pili kwa Compact Energies Limited kushinda kwa mwaka huu 2024.

Tuzo nyingine iliyoshinda mwaka huu ilikuwa tuzo ya BEST ENGINEERING COMPANY OF THE YEAR -EACOP PROJECT – Iliyotolewa nchini Afrika ya Kusini katika mashindano ya Solaris Africa(Solar Quarter) awards 2024 ( mwezi machi mwaka huu).

Lakini tayari kampuni hii ya Kitanzania imeshinda tuzo nyingine mbalimbali ikiwemo za (Solar African company of the year 2023 na winner of Jubilant Stewards of Africa Industrial Leadership Awards 2023 – Pace Setter Solar Supplier.

Akiongea baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Meneja Masoko na Mauzo wa Compact Energies Fred Pantaleo Msafiri amesema tuzo hizo zinatokana na utoaji huduma nzuri kwa wateja.

“Tumefanya miradi mbalimbali mikubwa pamoja na kuwafikia wananchi wanaohitaji Umeme Jua majumbani, mashambani katika mikoa mbalimbali ambao siku zote wamekuwa mabalozi wetu wazuri,

“Hii ni kwa sababu hatuiishii hapo tu, tukishawagungia, tunawapa garantii ya muda mrefu na huduma ya kufanya matengeneyo (service) pale inapohitajika,” amesema.

Amewataka Watanzania kutumia nishati jua katika kuendelea kuunga mkono azma ya serikali ya matumizi ya nishati safi na salama.

Tuzo hizo ziliandaliwa na kampuni ya Easternstar Consulting Group Tanzania Limited na kushirikisha zaidi ya nchi 23 barani Afrika ambapo makampuni zaidi ya 700 yameshiriki na 134 yamepata tuzo katika vipengele tofauti.

Akiongea baada ya utolewaji wa tuzo hizo, Mtendaji Mkuu wa Easternstar Deogratius Kilawe amesema tuzo hizo zinatoa fursa kwa makampuni mbalimbali hapa nchini kukua kiuchumi, kutambulika kimataifa na kuweka ushindani wa kibiashara na makampuni ya nje.
 

Viongozi wa Kampuni ya Compact Energies Tanzania, Meneja Masoko Fred Msafiri (kulia) na Ephraim Kimati (kushoto) wakipokea Tuzo ya Kampuni Bora Afrika ( ACOYA) baada ya kushinda katika kutoa huduma za umeme Jua katika vipengele vya Uhandisi, Ununuzi na Ujenzi. Tuzo hizo zilitolewa katika ukumbi wa  Super Dome  Masaki mwishoni mwa wiki.
 

Muonekeno wa Tuzo ya Kombe kwa Kampuni hiyo

Related Posts