Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), mdhamini Mkuu wa
Ligi ya Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premiere League) imeendesha
msimu wa pili wa program yake ya michezo kwa watoto inayofahamika kama
NBC Chanua Account Football Clinic inayolenga kuibua vipaji sambamba na
kuhamasisha wazazi kuweka akiba kwa ajili ya watoto wao. Hatua hiyo ni
muendelezo wa mkakati wa benki hiyo katika kukuza sekta ya michezo nchini
kupitia vipaji sambamba kutoa huduma jumuishi za kifedha kwa makundi yote
wakiwemo watoto.
Pia
walikuwepo baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars, Stumai
Abdallah na Fatuma Issa. Kupitia program hiyo
benki hiyo pia ilikabidhi zawadi mbali kwa washiriki ikiwemo jezi za ushiriki
pamoja na mipira. Aidha ilishuhudiwa watoto hao
wakipata wasaa kushiriki programu mbalimbali za kimichezo chini ya usimamizi wa
wachezaji hao wanaofanya vizuri kwenye sekta ya michezo hapa nchini ili
kuwafundisha mbinu mbalimbali za kimichezo.
Akizungumzia programu
hiyo iliyohusisha pia elimu kwa wazazi kuhusu fedha, umuhimu wa kuwawekea akiba
watoto na malezi yenye kutoa kipaumbele kwenye michezo na vipaji vya watoto, Meneja Masoko wa NBC
Alina Kimaryo alisema kupitia program
hiyo inayotarajiwa kufanyika angalau mara tatu kwa mwaka, walengwa ni watoto
wenye umri kuanzia miaka sita hadi kumi na tatu sambamba na wazazi au walezi
wao.
”Benki ya NBC
tunaamini katika imani kwamba kesho nzuri inaandaliwa leo. Kupitia program hii
ya Kliniki ya mchezo ya Chanua Akaunti tunaandaa kesho nzuri kwa watoto kupitia
vipaji vyao hususani vya kimichezo kwa kuzingatia ukweli kwamba michezo ni ajira. Pia tunaandaa kesho ya
Watoto kupitia kuhamasisha wazazi wajenge utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili
ya Watoto wao na hiyo ndio sababu hapa unaona kuna vyote viwili yaani michezo
na elimu ya fedha na akiba kwa wazazi,’’ alisema Alina.
Akizungumzia elimu ya
fedha na malezi ya watoto, Msimamizi wa Huduma za Elimu wa Benki ya NBC, Yoabu
Ndanzi alisema pamoja na kuwajengea uwezo na maarifa wazazi kuhusiana na
umuhimu wa kuwawekea akiba watoto wao pia inalenga kuwajengea uwezo wa kutambua
umuhimu wa michezo na vipaji walivyonavyo Watoto wao ili waviheshimu na zaidi
waone namna ya kuviendeleza.
‘Tunashukuru kuona
kwamba wazazi wengi kwenye darasa hili tayari wana uelewa wa kutosha kuhusu kuweka
akiba ndio maana tayari wameshafungua akaunti za chanua kwa ajili ya Watoto wao.
Tunajitahidi zaidi kuwaelewesha kuhusu kutambua umuhimu wa michezo na vipaji
vya watoto wao kwa kuzingatia ukweli
kwamba michezo ni ajira. Ili kuwahamasisha wazazi na watoto wenyewe tumewaletea
wachezaji mashuhuri kutoka vilabu vyao pendwa vinavyoshiriki ligi kuu. Tulianza
na wachezaji wa Azam FC, leo tumewaleta wa Simba SC na tukio lijali tutawaleta
wachezaji wa Yanga SC wakifuatiwa na wachezaji wat imu nyingine pia,’’ alisema.
Wakizungumzia hatua
hiyo wachezaji walioshiriki programu hiyo, pamoja na kuipongeza benki ya NBC
kwa jitihada zake katika kuendeleza mchezo wa soka hapa nchini, walionyesha
kufurahishwa zaidi na mpango huo kwa kuwa unatoa fursa kwao kushirikiana na
jamii hususani watoto, hatua ambayo itasaidia sana kuwashawishi wazidi kuupenda
mchezo huo sambamba na kuongeza juhudi zaidi waweze kufanikisha ndoto zao
kupitia michezo.
‘’Imekuwa ni furaha
sana kwetu hii leo na kwa hili tunawapongeza sana NBC kwa kuwa kupitia program
hii ya NBC Chanua Account Football Clinic wametukutanisha na watoto ambao
tumeweza kucheza nao, tumewaelekeza baadhi ya mbinu chache za kimichezo na
zaidi tumewahamasisha waendelee kupenda michezo sambamba na kuzingatia masomo
yao kwa kuwa elimu na michezo vinaweza kabisa sambamba.’’
‘’Zaidi kwa kuwa
program hii inahusisha wazazi tunaamini kabisa itasaidia kubadili mitazamo yao
kuhusu suala zima la kuheshimu vipaji vya watoto wao,’’ alisema mchezaji Shomari
Kapombe, beki wa timu ya Simba SC.
Kwa upande wao baadhi
ya wazazi walioshiriki tukio hilo wakiwa sambamba na watoto wao akiwemo Bi Tima
Mohamed na Bw Khamis Kakolwa walisema wamevutiwa zaidi na program ya NBC Chanua
Account Football Clinic kwa kuwa
imehusisha maeneo mengi muhimu yenye manufaa kwa watoto ikiwemo michezo, elimu
ya fedha na akiba, afya na malezi ya watoto huku pia ikitoa fursa kwa wazazi na
watoto kufurahia pamoja sambamba na wachezaji wanaowapenda kutoka Ligi Kuu ya
NBC.
Katika kufanikisha
program hiyo iliyofanyika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mapema hii
leo, benki hiyo ilihusisha wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wazazi na watoto
wao walioungana na baadhi ya wachezaji
vinara kutoka klabu ya soka ya Simba SC wakiwemo Shomari Kapombe, Mzamiru
Yassin, Ladaki Chasambi na Golikipa Hussein Abel. Pia walikuwepo baadhi ya
wachezaji wa timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars, Stumai Abdallah na Fatuma
Issa.
Programu hiyo ilihusisha
pia elimu kwa wazazi kuhusu fedha, umuhimu wa kuwawekea akiba watoto na malezi
yenye kutoa kipaumbele kwenye michezo na
vipaji vya Watoto.
Programu hiyo
ilihusisha utoaji wa vyeti vya ushiriki kwa washiriki wote.
Meneja Masoko wa NBC
Alina Kimaryo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wacheza wa Simba SC pamoja
na wachezaji wa timu ta Taifa ya wanawake Twiga Stars wakati wa programu.
Timu ya NBC na wadau mbalimbali
wa benki hiyo wakiwahudumia Watoto walioshiriki programu hiyo.
Aidha ilishuhudiwa
watoto hao wakipata wasaa kushiriki programu mbalimbali za kimichezo chini ya
usimamizi wa wachezaji hao wanaofanya vizuri kwenye sekta ya michezo hapa
nchini ili kuwafundisha mbinu mbalimbali za kimichezo.