Vodacom Tanzania yaibuka kidedea katika tuzo za kidijitali

KAMPUNI inayoongoza kwa huduma za teknolojia na mawasiliano nchini ya Vodacom, imetunukiwa tuzo na Kampuni ya Serengeti bytes kupitia programu ya Tanzania Digital Awards katika wiki ya ubunifu (Innovation week).

Kampuni hiyo ya Vodacom imejishindia tuzo katika vopengele vitano ambavyo ni:

· Kampuni bora ya simu nchini

· Kampuni ya simu inayotoa huduma bora zaidi nchini

· Applikesheni bora ya huduma za kifedha

· Tuzo ya ubunifu wa kidijitali katika Afya (m-mama)

· Tuzo ya ubunifu wa kidijitali katika sekta ya huduma za kifedha (M-Koba).

 Wafanyakazi
wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi wa
Vodacom Business Nguvu Kamando (wa pili kushoto) wakionesha tuzo
walizoshinda katika wiki ya ubunifu iliyoambatana na utoaji wa tuzo za
Tanzania Digital Awards ambapo Vodacom iliibuka kidedea kwa kunyakua
tuzo tano.

Mkurugenzi wa Vodacom Business Nguvu Kamando
(kushoto) akipokea tuzo ya kampuni bora ya simu iliyotolewa na kampuni
ya Serengeti bytes na kupigiwa kura na Watanzania

Mkuu wa idara ya Masoko wa Vodacom Business Aileen
Meena (kulia) akipokea tuzo ya kampuni ya simu inayotoa huduma bora kwa
Wateja hapa nchini.

 Meneja
wa mifumo mipya ya huduma za kifedha Brenda Msola (kushoto) akipokea
tuzo ya kampuni ya ubunifu wa applikesheni bora ya huduma za kifedha.

 Meneja wa mifumo mipya ya huduma za kifedha
Brenda Msola (kushoto) akipokea tuzo ya ubunifu wa kidijitali katika
sekta ya huduma za kifedha (M-Koba).

Related Posts