WAHITIMU CHUO KIKUU MZUMBE WAAHIDI KUJENGA VYOO SHULE YA MSINGI MZUMBE

Katika tambua umuhimu wa michezo shuleni Club ya mpira ya wahitimu chuo Kikuu mzumbe wameahidi kuchangia ujenzi wa vyoo na sehemu ya kubadilisha mavazi Kwa wasichana katika shule ya msingi Mzumbe iliyopo wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro

Hii ni sehemu ya mashirikiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na wahitimu waliowahi kusoma Chuoni hapo ambapo ni miaka nne mfululizo sasa wahitimu hao wamekuwa na tabia ya kurudi chuoni na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kupata miti pamoja na kufanya usafi

Dkt.Lucy massoi ni mkurugenzi wa kulugenzi ya Ukimataifaji Baraza la wahitimu chuo kikuu Mzumbe amesema Mpango mkakati wa Chuo hicho kuendeleza mashirikiano na wahitimu Ili wawe mabalozi Wazuri waweze kikitangaza Chuo kwenye maeneo waliopo

Kwa mwaka huu 2024 wahitimu hao wameshiriki zoezi la kupanda miti, kufanya usafi pamoja na kucheza michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa Pete, mpira wa miguu, kukimbuza kuku na kuvuta kamba.


Related Posts