Watu 6 mbaroni kwa kudakwa na meno ya tembo

Watu sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za  kukutwa na nyara za serikali aina ya meno ya Tembo vipande 12. Anaripoti Safina Sarwatt, Kilimanjaro…(endelea).

Katika taarifa yake kwa wandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, SACP Simon Maigwa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia operesheni ya ukamataji wa makosa mbalimbali iliyofanyika kuanzia tarehe 20 Mei 2024 hadi  2 Juni 2024.

Amesema kuwa katika msako huo watuhumiwa sita ambao ni wanaume walikamatwa tarehe 30 Mei 2024 majira ya saa 02:51 usiku huko kitongoji cha Kitoghoto Kata ya Kivisini Tarafa ya Jipendea, Wilaya ya Mwanga wakiwa na nyara za serikali meno ya tembo.

Amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana Askari wa hifadhi ya Taifa (TANAPA) waliwakamata watu wanne wanaume (majina yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) ambao kati yao wawili ni wakazi wa Arusha wawili, mmoja mkazi wa Mwanga na mmoja akiwemo  raia wa nchi jirani ya Kenya, wakiwa na mifuko miwili ya salfeti ndani ikiwa imebeba mbegu za alizeti katikati kukiwa na meno ya tembo vipande sita.

Katika tukio lingine ameswma tarehe 1 Juni 2024 majira ya saa 4:00 usiku huko maeneo ya Kileo kata ya Kileo tarafa ya Mwanga, wilaya ya Mwanga waliwakamata watu wawili wanaume, wote wakazi wa Mwanga wakiwa na begi ndani yake kukiwa na meno ya Tembo vipande sita.

Amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara tu taratibu za kiupelelezi zitakapokamilika.

Related Posts