MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA JIMBO LA KWAHANI WAPIGWA MSASA, WAHIMIZWA WELEDI

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Dkt.Zakia Mohamed Abubakar leo tarehe 04 Aprili, 2024 wakati akifungua mafunzo kwa Makarani waongozaji Wapiga Kura vituoni yanayofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba, Mjini Magharibi-Unguja Zanzibar.

MamaMakarani waongozaji Wapiga Kura vituoni wakila kiapo chankujitoa uanachama wa Chama cha siasa na kile cha kutunza siri kabla ya kuanza mafunzo yao.

Makarani hao wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo yao ya siku moja hii Leo.

Makarani hao wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo yao ya siku moja hii Leo.

Makarani waongozaji wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar wametakiwa kufanya kazi kwa weledi wanapotekeleza majukumu yao ya uchaguzi.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Dkt.Zakia Mohamed Abubakar leo tarehe 04 Aprili, 2024 wakati akifungua mafunzo kwa Makarani waongozaji Wapiga Kura vituoni yanayofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba, Mjini Magharibi-Unguja Zanzibar.

Mhe.Dkt.Zakia amewataka Makarani hao kufanya kazi kwa uadilifu na weledi na katika utendaji wa majukumu yao wanapaswa kuzingatia katiba ya nchi, Sheria za Uchaguzi na kanuni zake, maadili ya uchaguzi na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume.

Kabla ya kufungua Mafunzo hayo, Makarani hao wapatao 30 walikula kiapo cha kutunza Siri na Kujitoa uachama wa Chama cha Siasa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani Bi.Safia Iddi Muhammad.

Uchaguzi wa Jimbo la Kwahani unatarajia kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 08, Aprili, 2024.

Related Posts