Kocha Yanga kutua Kaizer Chiefs

MUDA wowote kuanzia sasa huenda kocha wa zamani wa Yanga, aliyepo kwa sasa FAR Rabat ya Morocco, Nassredine Nabi akatangazwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ili kurithi mikoba ya Molefi Ntseki aliyefutwa kazi.

Nabi amekabakiza mechi moja tu ya Ligi Kuu ya Morocco akiwa na FAR Rabat kabla ya kumaliza msimu na tayari inaelezwa ameueleza uongozi wa kikosi hicho kutosalia kwa msimu ujao.

Mwanaspoti linajua kocha huyo ana nafasi kubwa ya kutua Kaizer baada ya AmaKhosi kumhitaji tangu alivyoondoka Yanga mwishoni mwa msimu wa 2022/2023.

Dili lake la kwanza kwa AmaKhosi lilikwama kutokana na hitaji lake la kutaka kutua na benchi nzima alililokuwa nalo Yanga ndipo akaibukia Rabat.

Akiwa Yanga kocha huyo aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho na Ngao ya Jamii mara mbili mfululizo kila moja na kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kabla ya kumpisha Miguel Gamondi aliyetetea ubingwa wa Ligi na Shirikisho, huku Ngao akiipoteza kwa Simba.

Alikopita: Yanga, Al Merrikh, PDHA, Ismail, Al Hilal, Al Ahli Benghazi

Related Posts