Narendra Modi akosa wingi wa viti bungeni – DW – 05.06.2024

Licha ya Waziri Mkuu wa IndiaNarendra Modi kushinda muhula wake wa tatu mfululizo, lakini chama chake cha BJP hakikupata wingi wa wawakilishi bungeni kama kilivyotarajia ili kukiwezesha chama hicho kuiongoza India, sasa BJP kinahitaji kutafuta washirika kutoka vyama vingine vya kisiasa ili kuunda serikali ya mseto.

Chama cha Waziri Mkuu Narendra Modi, kimepoteza wingi wa viti bungeni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 katika Uchaguzi Mkuu wa India.

India Mumbai 2024 | Waziri Mkuu Narendra Modi kwenye kampeni ya uchaguzi
Waziri Mkuu wa India Narendra ModiPicha: Punit Paranjpe/AFP/Getty Images

Miongoni mwa nchi zilizompongeza Narendra Modi ni pamoja na China. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning, amesema nchi yake iko tayari kushirikiana na jirani yake huyo.

Soma Pia:Mpinzani wa Modi apiga kura huku akiishutumu serikali kwa kumlenga  

Matokeo yaliyotolewa rasmi hapo jana Jumatano na Tume ya Uchaguzi ya India yalionyesha kuwa vyama vinavyomuunga mkono Waziri Mkuu Narendra Modi, vimepata viti vingi kuliko chama cha National Democratic Alliance (NDA) katika uchaguzi huo mkuu uliomalizika baada ya kufanyika kwa muda wa wiki sita. 

Wagomea wa ubunge wa chama cha NDA waangushwa kwa wingi

Wagombea wa ubunge wa chama hicho cha NDA wengi wao waliangushwa hali iliyomsababishia Modi mashangao na kutokuamini. Waziri huyo Mkuu wa India aliamini kwamba chama hicho kingeshinda kwa kishindo kwa kupata viti zaidi ya 400 lakini haikuwa hivyo.

Muungano wa vyama vinavyokiunga mkono chama hicho cha NDA ambavyo kwa pamoja vinaunda chama cha BJP ulishinda katika maeneo bunge 294 pekee. Chama kinachotawala nchini India cha BJP chenyewe kimepata jumla ya viti 240 tu, ikilinganishwa na viti 303 katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2019.

India I Rahul Gandhi - Uchaguzi
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini India cha National Congress, Rahul Gandhi.Picha: Altaf Qadri/AP/picture alliance

Kwa hivyo chama hicho cha BJP sasa kinahitaji kutafuta uungwaji mkono na vyama vingine vya siasa ili kuweza kufikisha viti 272 au zaidi katika bunge lenye jumla ya viti 543 ili kiweze kuwepo madarakani.

Soma Pia: Kiongozi wa upinzani India awataka raia kupinga ‘udikteta’

Wakati huo huo, wafuasi wa chama kikuu chaupinzanicha Indian National Congress kinachoongozwa na Rahul Gandhi, walionekana kuwa na furaha licha ya chama chao kushindwa katika uchaguzi huo mkuu.

Vyanzo: DPA/AFP/RTRE

 

 

Related Posts