Yanga yalamba zawadi ya Tsh milioni 537.5 kutoka SportPesa

Club ya Yanga leo imepewa Tsh milioni 537.5 na Mdhani wao wa Mkuu SportPesa kama sehemu ya zawadi (bonus) ya kufanya vizuri katika msimu wa 2023/2024.

Hundi hiyo imepokelewa na Rais wa Yanga Hersi Said kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa Abbas Tarimba, hiyo ni kama motisha kwa Yanga ya kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri.

Yanga SC ndani ya msimu wa 2023/2024 wametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu, Ubingwa wa CRDB Bank Federation Cup pamoja na kufika hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF Champions League kwa mara ya kwanza baada ya miaka zaidi ya 20 kupita.

Related Posts