Na Mwandishi Wetu
TUME ya Taifa ya Ushindani (FCC) imesema itahakikisha inaendelea kumlinda mlaji nchini hususani bidhaa zinazotoka katika viwanda vya ndani na vile vya nje.
Uitiwaji saini kwa upande wa FCC umefanywa na Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa CTI Mhandisi Leodgar Tenga .
Mkurugenzi wa FCC Erio baada ya kusaini makubaliano hayo ya ushirikiano, amesisitiza lengo la kusaini makubaliano hayo ni kuhakikisha kila mmoja anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi kukuza viwanda na kudhibiti bidhaa bandia.
Amefafanua kwamba katika majukumu ya CTI kupitia sera na dira zao zinaonyesha ambavyo wanalenga kulinda mazingira mazuri ya kufanya biashara nchini kwa wenye viwanda kufikia matarajio yao na kukuza uchumi wa viwanda.
Pamoja na hayo amesema FCC wanaendelea kulinda na kushabihisha ushindani, hivyo wanahakikisha wanadhibiti vitu ambavyo vinaweza kuathiri wawekezaji hao ikiwemo ukiukaji wa sheria na makubaliano kuhakikisha havifanyiki.
Akielezea kuhusu sheria ya bidhaa bandia amesema, inazuia kupitia mipaka ya nchi na kutozalishwa nchini, ndiyo maana wamesaini makubaliano hayo kuhakikisha wanalinda uzalishaji huo wenye tija katika kukuza ajira, fursa ya uchaguzi wa bidhaa na kukuza uchumi.