IGP WAMBURA – JESHI LA POLISI LAWEKEZA KWENYE JAMII

Jeshi la Polisi limeendelea kuwekeza
kwenye jamii ili kuweza kubaini, kutanzua na kuzuia uhalifu kwenye maeneo
mbalimbali ambapo wananchi Pamoja na viongozi wa mtaa wametakiwa kuendelee
kushirikiana na Wakaguzi wa kata katika kudhibiti uhalifu.

Kauli hiyo imetolewa na MKUU wa Jeshi
la Polisi nchini IGP Camillus Wambura wakati akiwavalisha nishani maafisa,
wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 246 kutoka kanda ya Kusini yenye mikoa ya
Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa niaba ya Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt.
Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara Kanali Patrick Sawala amelimwagia sifa na Pongezi Jeshi la Polisi nchini
kwa kuendelea kuimarisha hali ya usalama ya Mkoa huo na wananchi kuendelea
kufanya shughuli zao katika hali ya usalama na amani.

Amesema vyombo vya ulinzi vimeendelea
kuhakikisha Mtwara inakuwa salama na hata wananchi na makundi mengine
mbalimbali wanakaribishwa kuja kuwekeza katika mkoa huo ambao ni rafiki kwa
uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Huku akitoa rai kwa wananchi
kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi
na usalana ili kudumisha amani iliyopo umoja na mashirikiano ambayo ni nyenzo
thabiti ya maendeleo.

Related Posts