MAPRO ndio wataanza kucheza mashindano ya Gofu yaliyoandaliwa na klabu ya Morogoro Gymkhana, yatakayoanza Juni 14-16, huku Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luongo akiweka wazi namna walivyopania mashindano hayo huku akikiri ugumu wa viwanja vya mchezo huo mkoani humo.
Mapro watacheza siku moja (Juni 14), ili siku mbili zitakazofuata (15-16) iwe zamu ya wachezaji wa ridhaa na Mzuka wa Gofu kupitia Mwanaspoti lilizungumza na Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luongo, amesema jinsi wanavyojiandaa kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa na ushindani.
“Viwanja vya Morogoro Gymkhana, vipo tisa hivyo mchezaji akimaliza tisa vya kwanza inabidi arudie tena, ili kufikia viwanja 18, pia havina green sehemu ya kumalizia, ya kwao ni ya udongo wanaita brown, hivyo tunapofanya mazoezi lazima akili ijue uhalisia wa kile tutakachokutana nacho.
“Wachezaji ambao ni wanajeshi, huwaombea kibali mapema, tunapewa mtu wa utawala atakayeandaa posho, malazi na tunapewa usafiri, tofauti na wachezaji wa ridhaa wanaojisimamia kila kitu.
“Kuna wakati mwingine wachezaji wa ridhaa, huwapa lifti ya usafiri, japo malazi na chakula hujitegemea mgano nikiondoka na kedi natakiwa kumlipia kila kitu na hufanya hivyo, kumpa motisha.”
Mashindano hayo ya kalenda ya Chama cha Gofu (TGU) itashiriki kama Kili Golf,, TPC, Arusha Gymkhana, Mufindi, Lugalo, Moshi Gymkhana, Dar na Moro.