BRELA wa tano gawio la Serikali kwa taasisi za umma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni, 2024, amepokea gawio la kiasi cha TZS Bilioni Kumi na Nane Mia Tisa Sabini na Tatu, Millioni Mia Nane Hamsini na Tatu Elfu, Mia Tano Kumi na Nne na Senti Ishirini na Saba tu (18,973,853,514.27) kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ikiwa ni utekelezaji wa utoaji gawio kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Sheria ya Msajili wa Hazina Sura 370.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Dkt Fred Msemwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa BRELA na Bw Godfrey Nyaisa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA.

Related Posts