KISHINDO CHA RAIS SAMIA MKOANI SINGIDA//BILIONI 93 ZIMETOLEWA UWEKAJI TAA, UJENZI BARABARA NA MADARAJA

Serikali imetoa kiasi cha takribani Bilioni 93 Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan madarakani kwa ajili ya miradi ya uwekaji taa za barabarani, Ujenzi na matengenezo ya Barabara, Pamoja na ujenzi wa madaraja.

Kiasi hicho cha fedha kimetolewa kwa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Singida ambapo umetekeleza miradi hiyo baadhi unaendelea na mingine imekamilika kwa wakati.

Akizungumzia utekelezaji wa miradi hiyo mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo yake Kaimu Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Singida Mhandisi Yohannes Mbagalo ameitaja miradi hiyo kuwa ni Pamoja na Uwekaji wa taa 51 za barabarani Mji wa Manyoni katika barabara kuu ya Kintinku – Singida – Malendi uliogharimu Shilingi Milioni 181,274,800.00 na mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Makongorosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa kwa kiwango cha lami; Lot 7(A) Sehemu ya Noranga – Itigi (Mlongojii), kilomita 25 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 29,770,297,740.00.

Mhandisi Mbagalo ameitaja miradi mingine kuwa ni Pamoja na Uwekaji wa taa 51 za barabarani katika Mji wa Ikungi katika barabara kuu ya Kintinku – Singida – Malendi wenye gharama ya Shilingi Milioni 181,274,800.00

Ujenzi wa jumla ya kilometa 1.7 kwa kiwango cha lami katika barabara ya Mkoa ya Ikungi – Londoni – Kilimatinde (Solya) kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 1,624,391,000.00. Mradi huu umetekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ya mradi kilometa 0.9 ilianza tarehe 30/8/2022 na kukamilika tarehe 25/5/2023 kwa gharama ya Shilingi Milioni 874,104,000.00 na awamu ya pili ya mradi kilometa 0.8 ilianza tarehe 12/9/2023 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30/6/2024 kwa gharama ya Shilingi Milioni 750,287,000.00

Mhandisi Mbagalo ameitaja miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitatu Katika Manispaa ya Singida ikiwa ni Pamoja na mradi unaoendelea wa Ujenzi wa utanuzi wa barabara kilometa 2.3 kutoka Skyway hadi eneo la Liti Mjini Singida katika barabara kuu ya Kintinku – Singida – Malendi kwa gharama ya Shilingi Bilioni 1,991,806,780.00.

Ujenzi wa daraja la chini (Underpass) Singida Mjini eneo la Kibaoni katika barabara kuu ya Kintinku – Singida – Malendi. Mradi huu ulianza kutekelezwa tarehe 30/8/2022 na kukamilika tarehe 25/6/2023 mwaka wa fedha 2022/2023 kwa gharama ya Shilingi Milioni 568,746,400.00.

“Mradi huo unaenda sambamba na mradi wa Upendezeshaji wa barabara kuu (Highway beautification) Singida Mjini eneo la mzunguko (Singida round about) katika barabara kuu ya Kintinku – Singida – Malendi” Amekaririwa Mhandisi Mbagalo

Mradi mwingine ni Ujenzi wa Madaraja ya mabwawa ya Kindai na Monangi pamoja na kunyanyua tuta la kilometa 1 pamoja na taa za barabarani (street light) katika barabara ya Mkoa ya Iyumbu – Mgungira – Mtunduru – Magereza kwa gharama ya Shilingi Bilioni 2,986,929,500.00. Mradi huu umetekelezwa kwa awamu mbili mfululizo.

Awamu ya kwanza ya mradi ilikua ni ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo ulianza tarehe 4/9/2022 na kukamilika tarehe 25/9/2023 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 2,733,239,500.00 na awamu ya pili ni ya mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo mradi huo ulianza tarehe 12/9/2023 na unatarajia kukamilika tarehe 30/6/2024.

Ameitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Barabara ya Sabasaba – Sepuka – Ndago – Kizaga kilometa 77.4 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Shilingi Bilioni 88,583,246,568.69. Utekelezaji wa mradi huu ulianza tarehe 10/11/2023 na unatarjiwa kukamilika tarehe 8/11/2025 mwaka wa fedha 2023/2024 na 2024/2025.

Ujenzi wa barabara mchepuko (bypass) na madaraja eneo la mlima Sekenke (Sekenke Escarpment) katika barabara kuu ya Kintinku – Singida – Malendi kwa gharama ya Shilingi Bilioni 37,800,000,000.00 ambazo zimekadiriwa kutumika kwa ajili ya kazi hiyo na mradi huu upo kwenye hatua za manunuzi.

Pia ameutaja mradi wa ujenzi wa Daraja la Mwajuma pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 1. Utekelezaji wa maradi huu ulianza tarehe 21/9/2023 na unatarajiwa kukamilika tarehe 25/6/2024 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 3,278,686,000.00.

Mhandisi Mbagalo amesema kuwa ujenzi wa mradi huo wa daraja la Mwajuma ni juhudi binafsi za mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mhe Dkt Mwigulu Nchemba ambaye amekuwa mstari wa mbele kupigania daraja hilo ili kuhakikisha linakamilika haraka.

“Mradi mwingine ni Ujenzi wa daraja la Msingi mita 100 na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 1 ikiwa ni pamoja na taa za barabarani (street light). Utekelezaji wa mradi huu ulianza tarehe 11/6/2019 na kukamilika tarehe 9/9/2022 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 11,143,018,612.” Amekaririwa Mhandisi Mbagalo

“Pia kuna mradi wa Ujenzi wa barabara za Mji wa Nduguti (km 10.0) kwa kiwango cha lami kiasi cha Shilingi Bilioni 22,900,000,000.00 ambazo zimekadiriwa kutumika kwa ajili ya kazi hiyo na mradi huu upo kwenye hatua za manunuzi” Amesisitiza

Kwa upande wake Msimamizi wa kitengo cha maabara ya udongo wa Wakala ya Barabara (TANROADS) Mkoa wa Singida Mhandisi Kitwana Rashid ameutaja mradi unaoendelea mpaka hivi sasa wa Ujenzi wa barabara ya Kitukutu – Gumanga – Mkalama – Nyahaa (5.0 km) ambao utajengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Shilingi Bilioni 5,362,958,200.00.

Related Posts