MSINGI WA ELIMU UMEBEBWA NA ELIMU YA AWALI NA DARASA LA KWANZA

Naibu katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu) Dkt Charles Msonde amesema Msingi wa Elimu ya Tanzania umebubwa na kujengwa katika msingi bora wa Elimu ya awali na darasa la kwanza hivyo walimu wanapaswa kuwa na usimamizi mkubwa na mzuri katika kuwafundisha wanafunzi hao ili wawe na msingi bora wa Elimu.

Dkt. Msonde amesema haya katika kikao cha Pamoja kati ya walimu hayo, Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule na wawakilishi kutoka Chama Cha Walimu Tanzania kilichofanyika katika Shule ya sekondari ya Hussein Bashe katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora.

“Katika shule za msingi kuna changamoto kazaa ambazo ni lazima ziondeke ili kuboresha elimu Tanzania miongoni mwao ni Watoto kumaliza elimu ya Awali na darasa la kwanza bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu. Jambo hili linapelekea kuua msingi bora wa Elimu ya mtoto huyo kwani Msingi wa Elimu umebubwa na elimu ya awali na darasa la kwanza”

Pia amewataka walimu kuweka Juhudi kubwa kwa wanafunzi wa darasa la Tatu kwani kitaalamu ndilo linaweka Msingi wa Ujuzi na Umahiri wa Masomo yote kwa Wanafunzi na sio kupambana na Darasa la Nne kama wanavyofanya sasa.

Dkt Msonde amewataka walimu kuzingatia mambo makuu manne mhimu ya kuzingatia wakati wa kufundisha Watoto ambayo ni kujua uwezo wa Watoto, kujua utayari wa Watoto katika kuyapokea yale unayoyafundisha, mazingira na umri wa Watoto ili kufanikisha zoezi la ufundishaji na ujifunzaji.

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Nzega Mhandisi Modest Aponary. Salim Mndolwa akitoa neno la shukrani amesema ofisi yake itahakikisha walimu wanapata stahiki zinazotakiwa ikiwa ni Pamoja na kulipa madeni ya Fedha za Uhamisho na Safari kwa wakati.

Related Posts