Sudan Kusini yakaribisha mechi ya kwanza kabisa ya kufuzu Kombe la Dunia mjini Juba

Rais wa FIFA Gianni Infantino alijumuika na Rais wa nchi hiyo, Salva Kiir Mayardit, na Rais wa FA Augustino Parek, kuadhimisha hafla fupi baada ya FIFA kuwekeza karibu dola milioni 7 (pauni milioni 5.49) kwa ajili ya uzinduzi wa Uwanja wa Taifa katika mji mkuu wa Sudan Kusini siku ya Jumanne.

Infantino alihudhuria mechi ya Sudan Kusini ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026 kwenye uwanja huo – ikiwa ni mara ya kwanza kwa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA kufanyika nchini humo.

‘Bright Stars’ ilichapwa mabao 3-0 na Sudan lakini hakuna kilichoweza kuchafua hafla hiyo.

“Leo, kwa mpira wa miguu, tunaunganisha ulimwengu, tunaunganisha Sudan Kusini, tunaunganisha Afrika, tunaunganisha watu wote wanaopenda mchezo wetu”, alisema Infantino.

“Tunafanya hivi hapa, katika mji mkuu wako, Juba. Nina furaha sana leo na ninajivunia kusaidia katika siku hii ya kihistoria, Juni 11, 2024 kwa mchezo wa kihistoria,” aliongeza.

Related Posts