WAKURUGENZI, MAAFISA ELIMU NA MAAFISA UTUMISHI SHIRIKIANENI KUTATUA KERO ZA WALIMU NCHINI

Naibu katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu) Dkt Charles Msonde amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini kushirikiana na maafisa Elilmu na maafisa Utumishi wa Halmashauri kutatua kero mbali mbali zinazowakabili walimu kote nchini.

Dkt. Msonde ametoa maelekezo hayo katika kikao cha Pamoja kati ya walimu wa shule za msingi na sekondari, Wakuu wa Shule wa Tarafa ya Ziba, Maafisa Elimu, Afisa kutoka Tume ya utumishi wa Walimu na wawakilishi kutoka Chama Cha Walimu Tanzania kilichofanyika katika Shule ya sekondari ya Ziba katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.

“serikali ya awamu ya sita ina agenda na walimu hawa ya kuboresha Elimu ya Tanzania, hatutaki wawe na changamoto mbalimbali kazi yao kubwa ni kufundisha Watoto wapate ujuzi, hivyo Wakurugenzi, Maafisa Elimu na Maafisa Utumish shirikianeni kutatua kero za Walimu Nchini”

Amewaelekeza walimu mbalimbali wenye changamoto kupeleka kwa wakuu wa Idara ya Elimu Msingi au Sekendori na wakuu wa Idara hizo kupeleka wao wenyewe kwa Wakuu wa Idara ya Utumishi, na kushirikiana kwa Pamoja kuzitatua.

Aidha Dkt Msonde amewataka walimu kuwa na tabia ya kurekebisha makosa yaliyofanywa na walimu waliotangulia katika kuwafundisha wanafunzi ili Watoto hao wawe na umahiri unaotakiwa katika kujifunza.

Amewataka walimu kote nchini kuendelea kutia mkazo katika kufundisha somo la Kingereza ili waweze kuwa na ujuzi mpana katika masomo mbalimbali hasa kwa wanafunzi wa sekondari kwani kwa sasa watahini wanazingatia katika umahiri wa Mwanafunzi.

Naye Afisa elimu sekondari wa Halmashauri ya Bw. Benjamin Siperto kwaniaba ya Mkurungezi wa halimsahuri ya Mji wa Igunga amesema maelekezo yote yaliyotolewa yataanza kufanyiwa kazi mara moja kwa kuwataka walimu kuanza kupeleka madai yao katika ofisi yake.

Related Posts