Kampeni ya tathmini ya lishe imeanza Leo rasmi ambapo watoto zaidi ya elfu mbili wenye umri chini ya Miaka miaka mitano wanatarajia kupata vipimo katika vituo vyote vya kutolea huduma ya Afya na katika vituo vinavyotoa huduma ya mkoba vilivyoanishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba ameeleza kuwa katika Halmashauri ya Iringa watoto sitini na nane elfu mianne na sabini na Tisa watapata huduma hiyo ,Manispaa ya Iringa ni watoto elfu arobaini na nne miamoja tisini na Saba,wilaya ya kilolo watoto elfu hamsini na Saba mia Moja arobaini na tatu ,mafinga mjini watoto elfu ishirini na sita mia sita hamsini na nane na wilaya ya mufindi watoto elfu sitini na mbili mia Saba ishirini na Saba wanatarajia kupata huduma hiyo.
Afisa lishe Mkoa wa Iringa Anna Patrick Nombo amezitaja huduma ambazo zitatolewa kuwa ni upimaji wa magonjwa sugu,uelewa wa masuala ya lishe Kwa wahudumu na wazazi pamoja na Hali ya ulemavu .
Aidha Afisa lishe ameongeza Kwa kusema kuwa changamoto ya utapiamlo imekuwa ikichangia vifo Kwa watoto wachanga na hii ni kutokana na Mama mjamzito kukosa lishe Bora kipindi Cha ujauzito hivyo kupelekea mtoto kuzaliwa na Udumavu na zoezi Hilo litaambatana na utoaji wa matone ya vitamini A.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Kheri James amewataka viongozi kulizungumzia suala la kutokomeza Udumavu Kila Mahali ikiwemo makanisani,mitaani na misikitini Ili watu waone umuhmu wa kupeleka watoto kupima na kuweza kufikia matarajio ya lengo la kampeni hiyo .
Kikao hicho Cha tathmini ya Hali ya Udumavu kinehudhuriwa na kamati ya usalama wa Mkoa wadau mbalimbali pamoja na viongozi wa dini na Mkoa imeunda timu ya wahudumu 343 watakaotoa huduma na Kwa Kila kituo kutakuwa na watumishi wanne na watoa huduma sita.