BALOZI NCHIMBI BUNGENI AKIFUATILIA BAJETI

Matukio mbalimbali katika picha, yakimuonesha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, akiwa ndani na nje ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kabla, wakati na baada ya kuwasilishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali iliyosomwa na Waziri wa Fedha, Ndugu Mwingulu Lameck Nchemba, leo Alhamis, Juni 13, 2024.

Balozi Nchimbi alimbatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania, Ndugu Ally Hapi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Ndugu Suzan Kunambi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Ndugu Jokate Urban Mwegelo.

Related Posts