IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP) kimetangaza kuwa kitashirikiana na chama tawala cha African National Congress (ANC) huku ANC kuunda serikali ya muungano itakayoweza kuongoza baada ya uchaguzi wa tarehe 29 Mei mwaka huu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Bunge jipya linatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza mjini Cape Town Ijumaa baada ya matokeo ya uchaguzi kuonyesha kuwa hakuna chama kilichopata ushindi wa kutosha.

Kiongozi wa chama cha Inkatha Freedom party, Velenkosi Hlabisa, akisalimia umati wa wafuasi wake wakati wa kampeni ya chama huko Richards Bay, tarehe 26 Mei 2024.

Chama cha IFP kilipata viti 17 katika bunge la taifa lenye viti 400 ambapo wabunge wataitishwa kumteua spika na kumchagua rais wa nchi.

ANC, kikiwa na viti 159, tayari kimeashiria kuwa kinataka serikali ya umoja wa kitaifa yenye kundi kubwa la vyama, kuanzia mrengo wa kulia hadi mrengo mkali wa kushoto.

“Ni wakati kwa IFP kuiimarisha serikali tena,” kiongozi wa chama Velenkosini Hlabisa aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

“Tunaweka mbele uthabiti na maslahi ya Afrika Kusini, kama tulivyoahidi kufanya wakati wa kampeni ya uchaguzi,” alisema.

Ameongeza kuwa “Katika serikali mpya, chama cha IFP kitaleta uadilifu, na msukumo wa kuendeleza nchi yetu na wananchi wetu kuelekea mustakabali bora.”

Vyama vya kisiasa vimekuwa vikijitahidi kujenga muungano baada ya chama cha African National Congress cha Rais Cyril Ramaphosa kupoteza wingi wa kura kwa mara ya kwanza katika uchaguzi huo.

Chama hicho kilipata asimilia 40 ya kura, ushindi mdogo kuwahi kupata, na sasa kinahitaji kuungwa mkono na vyama vingine ili kiweze kutawala.

Related Posts