Na Mwandishi Wetu
Baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Mohammed Ali Kawaida kuitaka Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kufungia Mtandao wa X ambao Zamani ulijulikana kama Twitter kutokana na mtandao huo kuruhusu mambo ambayo ni kinyume na Utamaduni wa Watanzania
Jukwaa la wanahabari wa mitandao ya Kijamii Tanzania(JUMIKITA) limeiomba Serikali ya chini ya Uongozi makini wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokubali kamwe kuingia kwenye mtego wa kufungia mtandao huo wa Kijamii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mweyekiti wa Jukwaa hilo amesema kuwa wakati wa sasa kufungia Mtandao sio jambo linalojenga afya kutokana na kuongezeka mifumo ya Teknolojia ya upatikanaji wa taarifa.
“Ni kama ilivyo Instagram ,Facebook na YouTube, ‘x’ au Twitter ni sehemu ambayo vijana wa Kitanzania wamekua wakilitumia Jukwaa hilo kujipatia riziki mfano Matangazo lakini pia hata Kazi nzuri za Serikali mbalimbali Wanahabari wa mtandaoni wamekua wakizichapisha ‘x’ “
“JUMIKITA ipo tayari kushirikiana na Serikali kujua namna bora ya matumizi ya mitandao ya kijamii na inatoa ushauri serikali isiingie kwenye mtego wa kufungia mtandao huo”amesema Matwebe
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA)Shaban Matwebe pichani