Mmiliki wa duka mbaroni akidaiwa kumlawiti mtoto wa miaka 14

Iringa. Jeshi la Polisi mkoani Iringa  linamshikilia mmiliki wa duka, Blass Nicholous (35) maarufu  Matowa mkazi wa Mtaa wa Kitasengwa, Kata ya Isakalilo Manispa Iringa  kwa tuhuma za kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 14.

Mfanyabiashara huyo anatuhumiwa kumlawiti  mtoto huyo ambaye ni mhitimu wa darasa la saba mwaka jana, baada ya kumpa  kazi ya kuuza duka.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Alfred Mbena amesema mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo nyumbani kwake Kitasengwa wakiwa wamelala.

Katika taarifa yake aliyotoa leo Juni 13, 2024 Kamanda Mbena amesema tukio hilo lilitokea Juni 9, 2024 saa tano usiku.

Amesema mtoto huyo alirudi nyumbani akitoka dukani kwa mwajiri wake ambaye ni mtuhumiwa na kwenda kulala katika chumba ambacho huwa wanalala pamoja taangu alipomwajiri kuuza duka hilo.

Amesema muda mfupi baadae alisikia mlango ukigongwa na alipofungua mtuhumiwa alikuwa amerejea hivyo alimfungulia akaingia ndani.

Kulingana na Kamanda, mtoto huyo akiwa amelala alishangaa kuona bosi wake anavua nguo zote kisha akapanda kitandani kulala.

Wakiwa wamelala pamoja mtuhumiwa huyo alianza kumvua suruali muhanga na kumuingizia uume sehemu ya haja kubwa ambapo alihisi maumivu makali ndipo alipoinuka kitandani na kwenda kulala sebuleni kwenye kochi.

Hata hivyo asubuhi ya Juni 10, 2024 mtoto alianza kuhusi maumivu ya tumbo lakini alioga na kwenda kazini kuuza duka.

Amesema akiwa dukani alikuja mama yake mlezi (Mama P) na kumweleza kitendo alichofanyiwa.

Kaimu Kamanda huyo amesema alimwambia  mume wake ambaye ni rafiki wa mtuhumiwa  na kisha kuwashirikisha viongozi wa serikali  ya mtaa kwa hatua zaidi.

Mbena amesema mtuhumiwa amehojiwa na kukana kuwa hajafanya kitendo hicho ambapo uchunguzi unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Related Posts