Mahakama ya hakimu Mkazi Wilaya ya Lindi imemuhukumu Mohamed Said Selemani mwenye umri wa miaka 62 mkazi wa kijiji cha Ng’apa wilaya ya Lindi, kwenda jela kutumikia kifungo cha maisha na kumlipa muhanga fidia ya shilingi 1,000,000 kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka 4 jinsia ya kiume.
Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Aprili 22,2024 huko kijiji cha Ng’apa Wilaya ya Lindi na kumsababishia maumivu makali mtoto huyo.
Hukumu hiyo ya kesi namba 11774 ya mwaka 2024 imetolewa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Maria Batulaine huku upande wa Jamhuri uliokuwa ukiongozwa na John Remi ambapo ulileta mashahidi watano pamoja na vielelezo karatasi ya Polisi fomu namba 3 (PF3) pamoja na cheti cha kuzaliwa.
Mtuhumiwa huyo alifikishwa kwenye mahakama hiyo Mei 06, 2024 na kusomewa shitaka lake ambapo alikana shitaka.