Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa akizungumza na Makundi ya Kianamama, vijana na makundi maalumu) wakati baraza hilo lilipoifikisha Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) mkoani Njombe kwa lengo la kutoa uwezeshaji kwa makundi hayo, watatu kutoka kusho ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe , Bw. Anthony Mtaka, wa pili kutoka kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, Bi.Judica Omari, wa tatu kutoka kulia ni Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake, Bi. Sophia Mjema na wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya NJombe, Bi. Kissa Kasongwa. Picha na Mwandishi wetu, Njombe.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa akizungumza na Makundi ya Kianamama, vijana na makundi maalumu) wakati baraza hilo lilipoifikisha Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) mkoani Njombe kwa lengo la kutoa uwezeshaji kwa makundi hayo. Picha na Mwandishi wetu, Njombe.
Na mwandishi wetu, Njombe
BARAZA la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kupitia Program ya Imarisha Uchumia na Mama Samia (IMASA) imejipanga kutoa uwezeshaji kwa makundi ya kinamama, vijana na makundi maalumu ya Mkoa wa Njombe ili waweze kuongeza uzalishaji wa mazao yenye masoko nje ya nchi yaweze chochea upatakanaji wa fedha za kigeni hapa nchini.
Hayo yalisemwa na Katibu Mtendaji,Bi. Beng’i Issa wakati alipokuwa akizunguza na makundi ya akinamama, vijana na makundi maalumu jana Mkoani humo, kuwa IMASA imalengo kutoa uwezeshaji kwa mazao wanayozalisha yawe chachu ya kupata fedha za kigeni.
“Mkoa huu wa njombe ni muhimu sana sababu wananchi wanazalisha mazao ya biashara ambayo masoko yake yapo nje ya nchi na hii inasaidia kutuingizia fedhaza kigeni katika taifa letu,” na aliongeza kusema IMASA imejipanga kuwawezesha ili waweze kuongeza uzalishaji.
Alisema mazao yanayozalishwa na kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi ni pamoja na kilimo cha miti kuzalisha mbao, kilimo cha zao la parachichi na vilevile mazao ya viazi na mazao hayo yanamasoko nje ya nchi.
Alisema mkoa huo ulipokea program hiyo vizuri na wengi walijitokeza kujiunga katika kanzi data ya baraza ukilinganisha na mikoa mingine ili kupata uwezeshaji na walioshiriki katika program hiyo ni wananchi 700.
Alifafanua kwamba mkoa huo unahalmashauri za wilaya nne na kila halmashauri iliwakilishwa vizuri ili kupata elimu namna ya kujiunga kwa ajili ya kupata uwezeshaji na kwenda kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara.
Alisema uwezeshaji unaohitajika ni kusaidia mazao wanayozalisha yaweze kuongezewa thamani, mfano mazao ya mbao takataka zake ziweze kupata mashine ya kuziendeleza ziweze kutumika kwa matumizi ya binadamu.
Pia alisema zao la parachichi linauzwa kabla halijaongezwa thamani nje ya nchi hivyo program itawezesha upatakanaji wa mashine kwa ajili ya kuliongezea thamani zao hilo kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Bw. Anthon Mtaka alisema programa hiyo imekuja wakati mwafaka na mkoa wake umejipanga kutekeleza na kuhakikisha matunda yake yanapatikana.
“Rais wetu wakati wote anazungumza biashara na uchumi hivyo na sisi wajibu wetu kumsaidia ili taifa hili liweze kusonga mbele kiuchumi,” sekta binafsi imepata kiongozi sahihi sababu ndiyo inayoajiri watu wengi alisisitiza.
Akitoa mfano alisema eneo linaloajili watu wengi ni kilimo, ufugaji na uvuvi na serikali imeweka ruzuku hivyo wananchi wanahitajika kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa huo kukuza mitaji na kuwa matajiri.
Pia aliwataka viongozi na watumishi mbalimbali katika mkoa huo wakatumie elimu hiyo kuwaelimisha wanachi kutumia fursa hiyo kuweza kuzalisha mazao kibiasharana kuondokana na umasikini na siyo kubaki maofisini bali wasaidie wananchi.
Alisema mkoa huo akinamama wanathubutu, wanauza viazi mviringo, wanashamba miti na anzalisha mbao na wanabodaboda na kwenye vumbi la mbao watengeneza bidhaa ni wachapakazi, kazi ni kuwaambia fursa hizo na mabenki kuwawezesha.
Mshauri wa Rais Katika Mambo ya Kinamama, Bi.Sophia Mjema alisema akinamama, vijana na makundi maalum wanahitajika kutumia IMASA ili kuweza kupata uwezeshaji na kuboresha shughuli za biashara na ujasirimalia.
Na Mwaanchi ,Bi.Sala Kile toka Wilaya a Njombe alisema anaamini kuwa programa hiyo itasaidia sana katika shughuli zao za ujasirishaji ili kuendeleza familia zao.