RC CHONGOLO AONGOZA MKUTANO WA BARAZA LA MADIWAN KUJADILI HOJA ZA CAG

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo ameshiriki Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe wa kujadili kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Mhe. Chongolo ameshiriki mkutano huo leo Jumanne Juni 11, 2024 ulilofanyika katika ukumbi wa Sambila uliopo kwenye ofisi za Halmashauri, ambapo hiyo ni mara ya kwanza kwa Mkuu huyo wa Mkoa kushiriki mkuano wa Baraza hilo tangu alipoteuliwa kuongoza Mkoa wa Songwe.

Katika mkutano huo, Baraza hilo limejadili hoja mbalimbali hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Mkutano huo pia, umehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda, Katibu Tawala wa Wilaya ya Songwe, ndugu Godfrey Kawacha, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Songwe pamoja na Wakuu wa Taasisi za Serikali wa Wilaya ya Songwe




Related Posts