TETESI ZA USAJILI BONGO: Nkane abadilishiwa upepo 2024-25

KLABU ya Mashujaa imeanza mpango wa kumsajili winga wa Yanga, Denis Nkane ili kuimarisha kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.

Nkane aliyejiunga na Yanga, Januari Mosi, 2022 akitokea Biashara United, lakini tangu atue kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho kwa misimu mitatu mfululuizo sasa, ameshindwa kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza chini ya aliyekuwa kocha, Nasreddine Nabi na hata sasa kwa Miguel Gamondi.

Kutokana na kukosa namna inaelezwa menejimenti ya mchezaji huyo imeona ni vyema kumfanyia mipango ya kuangalia sehemu nyingine itakayomwezesha kucheza ili kulinda kipaji alichonacho.

Mbali na Mashujaa, pia timu za Pamba ya Jiji, Ken Gold zilizopanda Ligi Kuu kwa msimu ujao zimekuwa zikitajwa kumnyemelea winga huyo aliyeanza kucheza kama beki.

Related Posts