VAR kutumika Ligi Kuu Bara

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, viwanja vitakavyotumika kwa michuano hiyo vitafungwa teknolojia inayomsaidia mwamuzi kufanya marejeo ya picha (Video Assistance Referee-VAR) kwa ajili ya kuhakikisha matokeo yanayopatikana yanakuwa ya haki.

Amesema katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, Serikali inakusudia kuwasilisha pendekezo la kuondoa kodi kwenye vifaa vinavyotumika kwenye teknolojia hiyo kuanzia mwaka mpya wa fedha 2024/2025.

Dk Mwigulu ameyasema hayo leo Alhamisi, Juni 13, 2024 wakati akisoma bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka mpya wa fedha 2024/2025.

“Tunataka matokeo yawe ya haki, sio kuna timu msimu unaisha imepewa penalti zaidi ya 10 na wengine mabao yao yanakataliwa, hivyo msimu ujao tunakwenda kutumia VAR,” amesema Dk Mwigulu

Related Posts