Viongozi wa nchi za G7 wakubaliana kuipa msaada Ukraine – DW – 13.06.2024

Kwa mwaka wa pili mfulilizo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy atahudhuria mkutano huo, akishiriki katika mazungumzo hayo leo Alhamisi.

Rais Zelensky amesema anatarajia “maamuzi muhimu” katika mkutano huo ambapo pia atatia saini makubaliano ya usalama na Japan na Marekani.

Viongozi wa G7 wanatarajia kutangaza angalau kimsingi mpango wa kuipa Ukraine mkopo wa dola bilioni 50  kwa kutumia riba inayotokana na mali za Urusi zilizozuwiwa baada ya uvamizi wake nchini Ukraine.

Tatizo la kisheria

Hata hivyo viongozi hao wanakiri kwamba mpango huo ni mgumu, huku wataalamu wa sheria wakitakiwa kushughulikia maelezo ambayo watahitaji ili kuungwa mkono na mataifa ya Ulaya, hasa Ubelgiji, ambayo siyo mwanachama wa kundi la G7.

Miongoni mwa agenda kuu za mkutano ni pamoja mzozo wa Mashariki ya Kati, uhamiaji na teknolojia za akili ya kubuni katika wakati ambapo wengi wao pia wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika mataifa yao.

Mwenyeji wa mkutano huu Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni pekee anaweza kushusha pumzi baada ya kushinda katika uchaguzi wa Ulaya Italia mwishoni mwa wiki.

Malumbano ya kibiashasa na China

Marais wa Marekani na Ukraine kutia saini mktaba wa ushirkiano wa kijeshi wa miaka kumi
Marais wa Marekani na Ukraine kutia saini mktaba wa ushirkiano wa kijeshi wa miaka kumiPicha: Presidential Office of Ukraine/ZUMA Press Wire/picture alliance

Katika kutilia mkazo azma ya Marekani kuiadhibu Moscow kwa sababu ya Uvamizi kamili dhidi za Ukraine, Washington siku ya Jumatano ilipanua vikwazo kwa Moscow, ikiwa ni pamoja na kulenga makampuni ya vifaa vya teknolojia ya China kuuza bidhaa zake kwa Moscow.

Kwa kutangaza vikwazo vipya kwa makampuni za China siku mmoja kabla za kuanza rasmi kwa mkutano wa G7, Biden bila shaka ana matumaini ya kuwashawishi washirika wa Magharibi kuonyesha dhamira kubwa katika kukabiliana na Beijing kuiunga mkono Urusi na hatua yake za kuzalisha bidhaa kwa wingi viwandani.

Huku haya zakijiri Italia inajaribu kupuuza tamko la G7 kuhusu uavyaji mimba kwa kuondoa marejeleo ya usitishaji “salama na wa kisheria.” Inaarifiwa kuwa  ya pingamizi kutoka kwa Waziri Mkuu wa mrengo wa kulia Giorgia Meloni kuhusu kulinda haki za ngono zimewakasirisha wanachama wa kundi hilo Uingereza, Canada, Ufaransa,Ujerumani, Japan na Marekani.

Ofisi ya Meloni jana Jumatano ilipinga haki ya utoaji mimba kupunguzwa kutoka kwa rasimu ya taarifa ya mwisho ya mkutano huo, ikisema mazungumzo yanaendelea.

Related Posts