Wafanyabiashara 42 wa Comoro kushiriki maonyesho ya Sabasaba 2024

Dar es Salaam. Wafanyabiashara 42 kutoka nchini  Comoro , wanatarajiwa kushiriki maonyesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, maarufu Sabasaba.
Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka katika viwanja vya Mwalimu Nyerere  jijini Dar es Salaam , ambapo taasisi, mashirika na kampuni mbalimbali huwa zikionyesha na kutangaza  bidhaa na huduma inazozitoa.

Katika taarifa yake aliyoitoa leo Alhamisi Juni 13,2024, Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu amesema  hii ni idadi kubwa ya wafanyabiashara  ambao wamewahi kujitokeza kushiriki maonyesho hayo kutoka nchini humo.

Amesema wafanyabiashara hao wanawakilisha sekta zinazojishughulisha na biashara ya vifaa vya ujenzi, nguo, kampuni za maji, vinywaji, wafugaji, vyakula vya mifugo, pamoja na bidhaa za kilimo hasa mazao ya mizizi.

Balozi Yakubu amesema ujio wa wafanyabiashara hao umetokana na juhudi za utekelezaji wa diplomasia ya uchumi na ubalozi wa Tanzania nchini Comoro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kufanikiwa kuwashawishi.

“Idadi hiyo ni kubwa kuwahi kujitokeza kutoka huku na wengi wao wanakwenda kwa lengo la kuangalia vyanzo vya usambazaji wa bidhaa za Tanzania zinazohitajika Comoro,” amesema Balozi Yakubu. 

Amezitaja bidhaa za Tanzania ambazo zina mahitaji na  soko kubwa Comoro kuwa ni  zana za kilimo, mazao ya kilimo, nyama, wanyama hai na  vyakula vya mifugo. 
Amesema  wafanyabiashara hao wameomba pia kupata fursa ya kufanya vikao na wafanyabiashara wa Tanzania pembeni mwa maonyesho hayo.

Aidha balozi Yakubu amesema  mameya wanane  wa miji mbalimbali ya kisiwa cha Anjouan nchini humo wanatarajiwa kufanya ziara kipindi hicho na watatenga muda kutembelea eneo la maonyesho.

“Kwa upande wa kipekee, ushirika unaojihusisha na uzalishaji wa mazao ya vanilla na langilangi unatarajiwa kushiriki. Hatua hiyo inatarajiwa kutoa fursa kwa wenyeji kujionea mbinu za uzalishaji na kuongezea thamani mazao hayo. Vanilla na langilangi ni mazao muhimu kwa kampuni zinazotengeneza manukato,”amesema Yakub.

Kwa mujibu wa balozi huyo, biashara baina ya Comoro na Tanzania imekuwa ikiongezeka katika miaka ya hivi karibuni ambapo mauzo ya Sh148 bilioni yalifanyika kwa bidhaa za Tanzania kwa mwaka 2023, huku biashara kubwa ikifanyika Julai hadi Desemba kila mwaka.

Pia nchi ya Comoro imekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia utekelezaji wa mikakati ya kuendeleza uchumi wa buluu kwa upande wa Tanzania.
Amesema takribani boti 100 za fiber husafirishwa kwenda Tanzania hasa Zanzibar, kila mwezi ambazo zina sifa kubwa kwa watumiaji nchini ikilinganishwa na boti kutoka kampuni nyingine.

SMZ kuongeza ushuru wa mvinyo, bia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imependekeza kuongeza kiwango cha kutozea ushuru wa bidhaa za vinywaji vikali ikiwemo bia.

Katika hotuba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya Salum kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025 amesema ushuru wa bidhaa kwa mvinyo utatoka Sh2,466 hadi Sh4,386 kwa lita moja.

Akisoma hotuba katika Baraza la Wawakilishi leo Juni 13, 2024 amesema ushuru wa bidhaa kwa vinywaji vingine vikali utapanda kutoka asilimia 35 hadi 70. 
Hatua hiyo amesema itaongeza pato la Serikali kwa Sh1 bilioni.

SMZ kuongeza ushuru wa mvinyo, bia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imependekeza kuongeza kiwango cha kutoza ushuru wa bidhaa za vinywaji vikali ikiwemo bia.

Katika hotuba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya Salum kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025 amesema ushuru wa bidhaa kwa mvinyo utaongezeka kutoka Sh2,466 hadi Sh4,386 kwa lita moja.

Akisoma hotuba katika Baraza la Wawakilishi leo Juni 13, 2024 amesema ushuru wa bidhaa kwa vinywaji vingine vikali utapanda kutoka asilimia 35 hadi 70. 
Hatua hiyo amesema itaongeza pato la Serikali kwa Sh1 bilioni.
Shisha, sigara za kielektroniki ushuru juu.

Kutokana na kuongezeka wimbi la matumizi ya shisha ‘sheesha’ na sigara za kielektroniki, hususan kwa vijana na watoto wadogo ambao ndio nguvu kazi ya Taifa imependekezwa kuongezwa kiwango cha ushuru kwa uingizaji wa bidhaa hizo Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya Salum akiwasilisha hotuba katika Baraza la Wawakilishi leo Juni 13, 2024 kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025 amesema Serikali inapendekeza kuongeza kiwango cha kutoza ushuru wa bidhaa kutoka asilimia 35 hadi asilimia 120 ili kuwalinda vijana, na watoto ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.

Related Posts