ANC yakubali kuungana na DA Afrika Kusini

Johannesburg. Baada ya vuta nikuvute kwa takribani wiki mbili, hatimaye Chama cha African National Congress (ANC) kimekubali kuungana na Democratic Alliance (DA) ili kuunda Serikali.

Mapatano hayo yamekuja zikiwa zimepita mbili tangu uchaguzi kufanyika Mei 29, 2024 ukishindwa kutoa mshindi atakayeunda Serikali.

Kwa mara ya kwanza tangu Serikali ya Wazungu wachache kusitishwa mwaka 1994, ANC ilishindwa kufikisha asilimia 50 ya kura na kupata asilimia 40.2, kikifuatiwa na DA (asilimia 22), kisha Umkhonto we Sizwe (asilimia 15) na Economic Freedom Fighters (asilimia 9.5).

Akizungumza na Shirika la Habari la Reuters leo Juni 14, 2024, mpatanishi wa DA, Helen Zille amesema mkataba umesainiwa kuunda serikali ya mseto.

Vyombo kadhaa vya habari vya Afrika Kusini pia vinaripoti mkataba umekamilika.

Mkataba wa mseto umethibitishwa ambao utamrejesha Cyril Ramaphosa kuwa Rais.

Kiongozi wa DA ambacho ni chama cha pili kwa ukubwa, John Steenhuisen, anasema hii ni sura mpya kwa nchi.

Wabunge wapya wameshaapishwa wakisubiri uchaguzi wa Spika wa Bunge.

Wabunge 400 wanatarajiwwa kuchagua Rais wa Afrika Kusini leo.

Related Posts