Dk Mwigulu atamani nembo ya Yanga kwenye noti ya Sh100

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema kwa mafanikio ambayo timu ya Yanga imeyapata anatamani kumshauri Gavana wa Benki Kuu (BoT) kuweka nembo ya klabu hiyo kama kungekuwa na noti ya Sh100 kuyaenzi mafanikio hayo.

Dk Mwigulu ametumia sehemu ya hotuba yake ya uwasilishaji wa Bajeti ya Serikali 2024/25 ya Sh49.3 trilioni jana Alhamisi, Juni 13, 2024 akizipongeza timu za Azam, Coastal Union, Simba na Yanga kwa kufanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Kimataifa.

Yanga na Azam zitacheza Kalabu Bingwa Afrika huku Simba na Coastal wakicheza Kombe la Shirikisho.

“Kwa umaalum kabisa nimpongeze GSM kwa uwekezaji mzuri alioufanya ambao umebadilisha kabisa taswira na uwezo wa kiuchezaji wa timu ya Yanga. Mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mzuri uliofanywa na GSM; GSM wewe ni mwamba, ujengewe sanam/mnara pale Makao Makuu ya Yanga,” alisema Dk Mwigulu.

Related Posts