Kagera Sugar inataka wapya 10

KAGERA Sugar inajipanga kuboresha kikosi chake kwa kupitisha panga kali ili kufanya vizuri msimu ujao, huku benchi la ufundi chini ya Fredy Felix ‘Minziro’ likipendekeza kuletewa wachezaji wapya 10.

Timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya 10 msimu ulioisha ikivuna pointi 34, huku ikilazimika kufanya maajabu katika mchezo wa mwisho kwa kushinda ugenini dhidi ya Singida Fountain Gate na kuepuka kucheza mechi za mtoano isishuke daraja.

Katika kufanya mabadiliko klabuni hapo, juzi (jumatano) uongozi wa Wakata miwa hao umetangaza kuachana na Mtendaji Mkuu, Ibrahim Mohamed baada ya mkataba wake kumalizika, huku ikianza mchakato wa kupata mrithi wake kwa ajili ya msimu ujao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Marwa Chambeli, alisema ripoti waliyoiwasilisha inajadiliwa na uongozi wa klabu hiyo walioahidi watatoa mrejesho na kuanza maboresho.

Alisema katika mapendekezo yao wanahitaji walau nyota wapya 10 wenye ubora katika maeneo yote kuanzia kipa, mabeki, viungo na washambuliaji ili kuleta ushindani tofauti na ilivyokuwa msimu ulioisha.

“Tumependekeza majina mapya 10,” Chambeli.

Related Posts