MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian akizungumza wakati akifungua kikao kikao cha Baraza Maalumu la kujadili Hoja ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) la Halmashauri ya wilaya ya Mkinga
Na Oscar Assenga, MKINGA.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian amehudhuria Baraza maalumu la Madiwani la hoja ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG) huku akizitaka halmashauri kwenye mkoa huo zenye hoja kuhakikisha wanazijibu na kufungwa kabla ya Juni 30 mwaka huu na ziwe zimepita kwa mkaguzi wa ndani na wa nje.
Balozi Batilda aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha Baraza Maalumu la kujadili Hoja ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) la Halmashauri ya wilaya ya Mkinga ambapo amesema kwamba hoja zilizopo nje ya uwezo wao na ambazo zinahitajika kuombewa kibali cha kufungwa waanze mchakato wa kuomba.
Alisema kwamba hoja zifutwe zifungwe za miaka ya nyuma lakini hoja za mwaka jana wanazokaribia saba nyengine karibia tisa hizo mpya tujitahidi ziweze kufutwa ziweze kuondolewa kwenye maeneo yenu..
“Lakini tuhakikishe hoja za CAG zinajibiwa na kufungwa kabla ya mwezi Juni 30, 2024 na zile ambazo zipo nje ya uwezo wenu na zinahitaji kujibiwa na zinajitaji kuombewa kibali cha kufungwa anzeni mchakato wa kuomba”Alisema RC Balozi Batilda.
Alisema katika Halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga ni Halmashauri 10 zimeweza kupata hati safi huku moja ya Kilindi ikipata hati ya mashaka
Aidha pia alisema kwamba Kuna fedha za miradi ya maendeleo ya vijiji wanazungumza uchaguzi wa serikali karibia milioni 68 ilitakiwa kwenye vijiji kwa ajili yay maendeeo ya vijiji huko sio kuchonganisha wenyeviti wa vijiji na wananchi.
“Hivyo nielekeze fedha zilizokuwa zinatakiwa ziende kuhakikisha zinapelekwa kabla ya Juni 30 mwaka huu na ziende zisimamiwe na ijulikae matumizi yake kwa lengo la kutumika kwenye malengo yaliyokusudiwa”Alisema
Jumla ya hoja 72 zilizotolewa katika Hesabu za CAG kwa mwaka 2022/2023 zikijumisha hoja za nyuma hoja 32 zimejibiwa na kufungwa huku hoja 40 sawa na asilimia 60 hazijajibiwa.