Wanachama maarufu wa Simba, Agness Daniel ‘Aggy Simba’ na Mohamed Hamisi ‘Dk Moo’ wamefungiwa na Sekretarieti ya klabu hiyo kujihusisha na masuala yote ya timu hiyo kutokana na malalamiko mengi ya kimaadili.
Sekretarieti ya Simba imewafungia wanachama hao hadi pale Kamati ya Maadili itakavyoamua vinginevyo.
Katika taarifa ya Simba kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo imeeleza kuwa, Sektretarieti imepokea malalamiko mengi ya kimaadili dhidi ya wanafamilia hao wa Simba ikiwemo kuitisha mikutano kinyume na utarqtibu ikiwemo kuchochea migogoro.
Sekretarieti itawafikisha wanachama hao mbele ya Kamati ya Maadili hivi karibuni .
Uamuzi huo umefikiwa kwa mamlaka iliyonayo sekretarieti iliyonayo chini ya ibara ya 31(4) (g) ya katiba ya Simba ya mwaka 2018 kama ilivyofanyiwa marekebisho 2024 katika kuhakikisha mahusiano ndani ya klabu, wanachama na mashabiki hayaathiriwi.
Sekretarieti inawakumbusha wanachama na mashabiki kuheshimu Katiba, Kanuni na miongozo iliyopo ndani ya klabu.