Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwamo Thobias Makoba kuwa Mkurugenzi wa ldara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wva Serikali. Kabla ya uteuzi, Makoba alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Makoba anachukua nafasi ya Mabhare Matinyi ambaye amepangiwa majukumu mengine. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni pamoja na Balozi Dk. John Stephen Simbachawene kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi, Balozi Dk. Simbachawene alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu.
Amemteua Nkoba Eliezer Mabula kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia utalii. Kabla ya uteuzi, Mabula alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu.
Aidha, CP. Benedict Wakulyamba atakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia maliasili.
Amemteua Dk. Habib Gallus Kambanga kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi, Dk. Kambanga alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu.
Amemteua Ally Rajab Mketo kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe. Kabla ya uteuzi, Mketo alikuwa Afisa Tawala Mwandamizi, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe.
Mketo anachukua nafasi ya Onesmo Kisoka ambaye amestaafu.
Amemteua Jaji Dk. Mary Caroline Levira kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. Jaji Dk. Levira ni Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Jaji Dk. Levira anachukua nafasi ya Jaji Dk. Gerald Nika ambaye amemaliza muda wake.
Amemteua Dk. Leonard Douglas Akwilapo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Dkt. Akwilapo ni Katibu Mkuu Mstaafu na Mhadhiri Mwandamizi, Kikuu Kikuu cha Dodoma.
Dk. Akwilapo anachukua nafasi ya Irof. Maurice Mbago ambaye amemaliza muda wake.
Amemteua Dk. Noel Euscbius Mbonde kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya Chuo cha Ufundi Arusha. Dkt. Mbonde ni Mkurugenzi Mstaafu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.