TANZIA: BALOZI RUHINDA AFARIKI DUNIA, KUZIKWA JUMATATU DAR ES SALAAM

Balozi wa zamani wa Tanzania katika nchi za Canada na Jamhuri ya Watu wa China na mhariri maarufu wa vyombo vya habari nchini, Ndugu Ferdinand Kamuntu Ruhinda, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Ruhinda ambaye alipata kuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya CCM ya Uhuru na Mzalendo, na yale ya Serikali ya Daily News/Sunday News na habariLeo kwa nyakati tofauti, atazikwa Jumatatu, Juni 17, 2024 kwenye makaburi ya Kondo, Kunduchi, mjini Dar es Salaam.

Ndugu Ruhinda ambaye pia alikuwa mwanzilishi wa magazeti ya Mwananchi na Redio Uhuru amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu akikakabiliwa na maradhi ya kisukari. 

Msiba uko nyumbani kwake, Masaki mjini Dar Es Salaam na taarifa zaidi kuhusu msiba huo itatolewa baadaye leo Jumamosi, Juni 15, 2024. 

Related Posts