TETESI ZA USAJILI BONGO: Waarabu kutibua dili la Aziz KI, Simba yahamia Burkina Faso

WAKATI Yanga wakipambana kumbakiza, Stephane Aziz Ki ambaye ndiye kinara wa upachikaji wa mabao msimu huu (21) inaelezwa Pyramids FC ya Misri imeonyesha nia ya kumuhitaji staa huyo.

Yanga na Aziz Ki walithibitisha kuendelea kupiga kazi pamoja, japo bado hajasaini mkataba na Pyramids imetuma ofa.

KLABU ya Simba imetajwa kufanya mazungumzo na beki wa FC Lupopo, Valentin Nouma raia wa Burkina Faso kwa lengo la kutaka kumsajili. Beki huyo wa kushoto (24) anatajwa kama mbadala wa Joyce Lomalisa aliyekuwa akipigiwa hesabu na kabla ya Lupopo alishakipiga Rahim FC na AS Douanes za Burkina Faso.

BAADA ya kuipandisha Pamba Jiji kucheza Ligi Kuu Bara aliyekuwa kocha mkuu wa chama hilo, Mbwana Makatta yuko hatua za mwisho kujiunga na Tanzania Prisons.

Pamba ipo katika mchakato wa kusaka kocha mpya sawa na Prisons iliyoachana na Ahmed Ally anayetajwa kutimkia JKT Tanzania, huku Makatta likitajwa kwa maafande hao sambamba na Songea United (FGA Talents).

KIUNGO mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Mghana Christian Zigah huenda msimu ujao asiwe sehemu ya kikosi hicho baada ya kumaliza mkataba. Hakuna mazungumzo yanaendelea baina ya Dodoma na Zigah na tayari kiungo huyo wa zamani wa Biashara United aliyemaliza msimu ulioisha akifunga mabao matatu na ameondoka Dodoma akiwa safarini kurudi Ghana.

KIUNGO mkabaji aliyemaliza mkataba na KMC, Masoud Abdallah ‘Cabaye’, ameingia katika rada za maafande wa Mashujaa na Tanzania Prisons, wanaohitaji huduma yake kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano. Imeelezwa mchezaji huyo, anaangalia ni timu gani itakuwa na masilahi yatakayomridhisha kisha akasaini.

BEKI wa zamani wa Singida Fountaine Gate, Carno Biemes anatajwa kujiunga na Al-Hamriyah FC ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).Endapo dili la Biemes litakamilika basi atatua kama mchezaji huru kwani ameshaliza mkataba na Singida na tayari ameshaangaa kabisa mashabiki wa timu hiyo.

STRAIKA wa KVZ na kinara wa mabao wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), Suleiman Mwalim Abdalla ametajwa kupigiwa hesabu na JKT Tanzania iliyonusurika kushuka daraja sambamba na Mashujaa.

Nyota hiyo mwenye mabao 20 ZPL inaelezwa amekuwa katika hesabu za JKT na Mashujaa na wanasubiri Ligi iishe Zenji.

Related Posts