Kilimo cha parachichi kuwainua wananchi Gairo

Mkuu wa wilaya ya Gairo Jabiri Makame amesema Katika kuendelea kuwainua wananchi kiuchumi wameendelea Kutoa Elimu ya kilimo Bora na kilimo misitu Cha zao la. parachichi ili kujikomboa kupita sekta hiyo

Jabiri amesema Wilaya hiyo ni Wilaya changa hivyo inahitaji nguvu ya ziada Ili kusukuma maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja hivyo kupitia Kilimo Serikali itaendelea kuwasapoti Kwa kuwapatia elimu,mbegu na masoko

Anasema Wilaya hiyo imekua inatekeleza program mbalimbali za Mazingira kwnye upandaji wa Miti akiwemo Urithi wa Kijani Gairo huku wananchi wakiitikia Wito huo hivyo wameona kutumia fursa hiyo kupanda Miti yenye faida ambayo itatunza Mazingira pamoja na kuwaingizia kipato.

Anasema katika kuendelea na program hizi wilaya imekua na Mazao ya kimkakati kama.parachichi na tumbaku huku mazao ya asili nayo kama alizeti,viazi na mahidi yakiendelea kulimwa.

Katika kuunga mkono zao hilo taasisi isiyo ya kiserikali Agri Wezesha inafika na mradi wa uhifadhi mazingira kiuchumi kupitia program ya kilimo misitu na urithi wa kijani Gairo na kugawa Miche ya Miti ya Parachichi zaidi ya Laki moja pamoja Miche ya Miti ya mbao.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Deogracia Ignas anasema wamekusudia kugawa Miche hiyo Ili kulinda Hali ya uharibifu wa mazingira pamoja na kuwainua kiuchumi wananchi.

Anasema kuwa Mradi huo utatelekezwa Kwa kipindi Cha miaka minne katika wilaya hiyo akitoa Wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo.

Related Posts