Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Klaus Chilima. Ibada ya Mazishi hayo imefanyika katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi.
Akitoa salamu za rambirambi, Makamu wa Rais amesema Tanzania inatoa salamu za pole na kuungana na waombolezaji wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki kigumu.
Makamu wa Rais amesema Hayati Chilima alikuwa kiongozi imara, mwanamajumui wa kweli wa Afrika ambaye wakati wote alitanguliza mbele maslahi ya wananchi anaowaongoza na Afrika kwa ujumla.
Pia Makamu wa Rais amemtaja Hayati Chilima kama kiongozi aliyesimamia umoja, amani na usalama, mageuzi ya kiuchumi ya Malawi na utawala wa kidemokrasia nchini humo.
Makamu wa Rais amesema wananchi wa Malawi na Ukanda wote kwa ujumla wanapaswa kumuenzi Hayati Chilima kwa kuendeleza yale aliyosimamia na kuendelea kumuombea apumzike kwa amani.
Katika kushiriki Mazishi hayo ya Kitaifa Makamu wa Rais ameambatana na Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Hamza Hassan Juma, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato pamoja na Balozi wa Tanzania Mhe. Agnes Kayola.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi kushiriki Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Chilima leo tarehe 16 Juni 2024. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Agnes Kayola na Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Rais Mstaafu wa Malawi Mhe. Dkt. Joyce Banda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi kushiriki Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Chilima leo tarehe 16 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi kushiriki Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Chilima leo tarehe 16 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa heshima za mwisho wakati akiaga mwili wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Chilima katika Mazishi ya Kitaifa yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi leo tarehe 16 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki katika Ibada ya Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Chilima katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi leo tarehe 16 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa salamu za rambirambi wakati wa Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Chilima katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi leo tarehe 16 Juni 2024.