Mchezo wa mkondo wa pili wa Play Off kati ya Tabora United dhidi ya Biashara United Mara unachezwa leo katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mchezo huo utategua kitendawili cha nani atacheza Ligi Kuu Bara na Ligi ya Championship msimu ujao 2024-25.
Mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Karume mkoani Mara, Biashara United ilipata ushindi wa 1-0.
Biashara United inasaka nafasi ya kucheza Ligi Kuu Bara ikitokea Ligi ya Championship, huku Tabora United ikipambana kubaki Ligi Kuu kwa msimu ujao na kama itashindwa itashuka daraja.