NJOMBE YAPOKEA MWENGE, LUDEWA YAANZA KUUKIMBIZA.

Mwenge wa Uhuru umepokelewa rasmi Mkoani Njombe katika Wilaya ya Ludewa ukitokea mkoani Ruvuma ambapo katika mkoa wa Njombe utakimbizwa Km. 726 na kupitia miradi yenye thani ya Tsh. Bil. 15.9.

Wilaya ya Ludewa ndiyo Wilaya ya kwanza kuanza kuukimbiza mwenge huo katika mkoa wa Njombe ambapo itakimbiza umbali wa Km. 137 mpaka kukabidhiwa kwake Juni 17 mwaka huu katika Wilaya ya Njombe na itapitia miradi 7 ambayo mpaka kukamilika kwake itagharimu kiasi zaidi ya Tsh.9.6.

Mbio za mwenge huo unaoongozwa na mkimbizaji kitaifa Godfrey Mzava ambapo utazindua miradi miwili, kukagua miradi mitatu na kuweka jiwe la msingi katika miradi 2.

Aidha katika kuzingatia jumbe mbalimbali za mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 katika eneo la mkesha zitatolewa taarifa mbalimbali za lishe, uchaguzi wa Serikali za Mitaa, dawa za kulevya, damu salama na upimaji wa VVU na ukimwi, taarifa ya Malaria, taarifa ya wajasiliamali pamoja na mdahalo.


Related Posts