Waziri Mkuu wa Tanzania Mh KASSIM MAJALIWA amesema uwepo wa kiwanda cha kutengeneza virutubishi vya vyakula

Waziri Mkuu wa Tanzania Mh KASSIM MAJALIWA amesema uwepo wa kiwanda cha kutengeneza virutubishi vya vyakula hapa nchini utasaidia kuimarisha afya za watoto na kupunguza vichwa vikubwa huku serikali ikiendelea kuhamasisha matumizi ya vyakula vyenye virutubishi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akifungua kiwanda kipya na cha pili barani Afrika cha kuzalisha virutubishi vya vyakula pamoja na kuzindua jukwaa la warutubishaji wa vyakula jijini Dar es salaam.

 

Pia, Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Afya,Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na wadau wote wa lishe washirikiane katika kuandaa mkakati mahususi wa kueleimisha umma na kuhakikisha wananchi wanatapata uelewa mpana wa umuhimu wa virutubisho vinavyochanganywa kwenye chakula katika kukabiliana na changamoto za lishe duni.

Ametoa maagizo hayo jana Jumamosi tarehe 15 wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kutengenenza virutubishi na tovuti ya wasindikaji chakula Tanzania kilichopo Mikocheni jijini Dar es salaam.Asema ili kulinda afya za walaji,wasindikaji wote wazingatie namna ya kutunza virutubishi na vinyunyizi vya virutubishi ili visiharibike.Kiwanda hicho ni cha kwanza kwa Afrika mashariki na cha pili kwa Afrika.

Amesema urutubishaji huo utaimarisha afya ya watoto wa kike waliokatika rika la balehe kwa kuwapunguzia changamoto ya upungufu wa damu,vile vile utasaidia kuimarisha afya za watoto kwa kukabiliana na tatizo la kupungua kinga mwilini ambalo ni chanzo cha watoto kuugua mara kwa mara,lakini pia kupunguza matatizo ya vichwa vikubwa,mdomo sungura na mgongo wazi kwa watoto.

Related Posts