KATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan mbali na kuwatakia kheri Watanzania katika sikukuu hiyo, pia ameshiriki Dua ya pamoja na waumini wa dini ya Kiislam baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Al Adha iliyosaliwa katika Msikiti wa Mikocheni kwa Warioba Jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Juni 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kupitia ukurasa wake wa X, Rais Samia ameandika; Nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Eid Al Adha. Ikawe siku njema kwetu sote yenye amani, umoja na upendo kwa jirani, ndugu, jamaa, marafiki na wote wenye kuhitaji ukarimu wetu.
“Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na baraka azipokee dua zetu, atusamehe makosa yetu, aendelee kutushika mkono na kutuongoza katika mema, kweli, haki na weledi katika kumtumikia yeye na wenzetu. Eid-al-Adha Mubarak,” ameandika Rais Samia.