TETESI ZA USAJILI BONGO: Najim kutoka Tabora kwenda Singida BS

SINGIDA Black Star imeweka dau la Milioni 130 ili kuipata saini ya kiungo wa Tabora United Najim Mussa, ikizilaza chali Simba na Azam.

Kiungo huyo ambaye bado anamkataba wa mwaka mmoja na nusu na Tabora katika msimu wake wa kwanza Ligi Kuu amecheza kwa mafanikio na kuzifanya timu kubwa tatu kugongana mlangoni zikiwania saini yake.

Simba hapo awali iliweka dau la Milioni 30 na baadae kuongeza mpaka 50, lakini ilisema hayo kwa mdomo tu huku Azam ikifika mezani kwa dau la Milioni 40.

Taarifa zinasema baada ya Singida kuweka dau kubwa zaidi ya vigogo hao wawili wa ligi, Tabora ilikubali kumuachia mchezaji huyo na baada ya kumaliza mechi ya juzi kwenye mechi ya Mtoano dhidi ya Biashara United alikwenda kusaini mkataba mpya na Singida. Mwanaspoti limeambiwa dili hilo limeiva.

Related Posts