Uzimaji Intaneti ni ukiukwaji wa haki za binadamu

WANAHARAKATI vijana nchini Tanzania wamesema kitendo cha Serikali kuzima intaneti wakati wa uchaguzi mkuu wa 2020, kimekiuka mikataba ya kimataifa pamoja na Katiba ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar ea Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki Binadamu na Utawala wa Kisheria ya Reach Out Tanzania, Kumbusho Dawson amesema kitendo cha serikali kutochukua kwa yeyote, kimetia shaka utawala bora wa sheria.

Alitoa kauli hiyo wakati akichangia mjadala wa  pamoja kati Asasi za Kirai, Watetezi wa Haki za Binadamu pamoja na waandishi wa habari.

Alisema uwepo wa mitandao ya kijamii unaendana na ukuaji wa teknolojia katika dunia ya sasa hivyo endapo itazimwa itakuwa imekiuka haki za binadamu ambazo zipo kikatiba.

”Tumekutana hapa kujifunza, kuzungumza na kushauriana juu ya kuzuia au kusema hapana uzimaji wa mitandao ya kijamii nchini,” alisema na kuongeza;

”Mtandao unapozimwa unaharibu uchumi wa watu wengi ikiwemo watu kukosa ajira, kutofanya biashara zao mfano watu wa Bolt na wanafunzi kushindwa kujisomea kwa kutafuta material.”

Alisema nchi inapoelekea katika uchaguzi ni vema kuhakikisha mtandao wa kijamii inaendelea kuwepo ili kuifanya jamii kushindwa kujua kinachoendelea.

Dawson alisema uzimwaji wa mtandao unakiuka katiba ya nchi ibara ya 18 ambayo inazungumzia haki mbalimbali ikiwemo haki ya kupata taarifa na haki ya kuzungumza na haki ya kujumuika.

Kwa upande wake, Mwanasheria kutoka Lawdowns Consult, Alphonce Lusako alisema katika dunia ya sasa mtandao ni sehemu ya binadamu.

“Kuna mkataba wa Umoja wa Mataifa wa 2018 umetambua  haki ya upatikanaji wa intaneti kama haki za binadamu, pia kuna African Declaration on Internet right ambao ni sehemu ya  binadamu, hivyo uzimwaji wa mtandao 2020 ulivunja sheria za ndani, Katiba ya nchi na mikataba ya kikanda na umoja wa kimataifa,” alisema.

Naye Mmoja wa wadau wa Global Member Advasory Board Gendem, Dorcas Francis alisema mtandao unapozimwa kuna madhara mengi yanaweza kujitokea hususan watu kukosa taarifa kwa ufasaha kuhusu masuala mbalimbali.

Related Posts