Stoltenberg amesema serikali ya Kyiv inahitaji ufadhili wa kijeshi unaooleweka na thabiti huku akipigia chapuo kuongezwa kwa mafungu katika bajeti za ulinzi za mataifa wanachama wa NATO kutokana na mashaka ya Donald Trump katika kuisaidia Ukraine.
NATO mwezi ujao inaadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwake kwa mkutano wa kilele utakaofanyika mjini Washington ambao unalenga kutuma ujumbe madhubuti wa kuiunga mkono Ukraine kabla ya Rais Joe Biden kuchaguliwa tena kuwania kiti cha urais mwezi Novemba dhidi ya mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump.
China na lawama za kuendeleza vita vya Urusi na Ukraine
Stoltenberg ameitupia lawama China kwa kuzidisha mzozo kati ya Urusi na Ukraine kupitia kile maafisa wa Marekani wanasema ni kutoa msukumo mkubwa wa mauzo ya nje kwa shabaha ya kujenga upya sekta ya ulinzi ya Urusi.
Nikimnukuu hapa anasema Rais Xi Jinping “amejaribu kujenga hisia za kujiweja nyuma katika mzozo huu, ili kuepusha vikwazo na kuendeleza biashara. Lakini kiuhalisia ni kwamba China ipo katika jaribio la kutimiza malengo mawili kwa wakati mmoja, kwa kuiunga mkono Urusi kwa upande mmoja huku ikijaribu pia kudumisha uhusiano na mataifa ya Magharibi.
Amesema serikali ya Beijing haiwezi kudhibiti vyote, na kama haitabadiliki mkondo wake itapaswa kukabiliwa na ipasavyo kwa kitendo hicho. “Kuna mazungumzo yanayoendelea miongoni mwa washirika wa NATOkuhusu jinsi ya kukabiliana na matokeo ya usalama kutona na ukweli kwamba China inaunga mkono juhudi za vita za Urusi nchini Ukraine.” Alisema Stoltenberg.
China yakana tuhuma za uchochezi
China hata hivyo imetetea uhusiano wake na Moscow na kuzitaja ripoti za Marekani kama upotoshaji. China imekwenda mbali zaidi na kusema, haitoi msaada wa silaha kwa pande yoyote katika mzozo kati ya Urusi na Ukraine, tofauti na inavyofanya Marekani na washirika wake wa Magharibi.
Aidha Stoltenberg ameongeza kuseama ziara ya Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Korea Kaskazini, ambayo inaipa makombora Moscow licha ya kuwa chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa, inaonyesha wazi jinsi gani serikali ya Moscow “ilivyokuwa tegemezi” kwa viongozi wa kimabavu.
Soma zaidi:Marekani yaidhinisha Ukraine itumie silaha kuyashambulia maeneo ya Urusi
Mkutano wa kilele wa NATO wa 2014 uliweka lengo la ufadhili ambalo lilifikiwa na nchi tatu pekee ambazo Marekani, Uingereza na Ugiriki, lakini pamoja na mambo mengine muhimu mkutano huu wa sasa wa Washington tofauti na wanachama 32 wa muungano huo pia utaleta washirika wanne muhimu kutoka Asia-Pacific: Australia, Japan, New Zealand na Korea Kusini.
Chanzo: AFP