KUAMBIANA INVESTMENT WAALIKA WATEJA WAO KWENYE BONANZA

KAMPUNI ya Kuambiana Investment yandaa Bonanza Kwa ajili ya Kuwakutanisha karibu wateja wao na kuweka Sawa Miili yao Kwa Michezo mbalimbali .

Akizungumza na Wanahabari Makao Makuu ya ofisi ya Kuambiana Sinza Jijini Dar es Salaam Meneja wa Kampuni hiyo Anna Minja amesema Wanatambua mchango mkubwa kutoka kwa Wateja wao ambao wamekuwa wakishirikiana nao kwa takribani Miaka 17 tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo.

Aidha amesema Bonanza hilo litafanyika Juni 30,2024 Katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam huku Mgeni rasmi wa Bonanza hilo akiwekwa kwenye mabano .

Pia amesema katika Bonanza hilo kutatolewa zawadi mbalimbali huku burudani ikisindikizwa na Wasanii na Michezo mbalimbali.

Kwa Upande wake Msaidizi wa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Charles Peter amesema Kampuni hiyo inathamini kwa 100% na kuunga Mkono Serikali kwa kutoa ajira kwa Vijana na hivyo kutokana na Mahitaji na ukubwa wa Kampuni hiyo Vijana 100 wamepata ajira .

Nae Mratibu wa Mashindano ya Kuambiana Cup John Richard ameeleza kuwa Mashindano hayo yamekuwa na muamko mkubwa sana kwa vijana kushiriki ambapo kumekuwepo na utofauti mkubwa kuanzia kwa washiriki hadi Mikoa iliyojiunga na Mashindano.

“Kuambiana Cup ilianzishwa mnamo 2021 ikiwa na Timu shiriki 09 Mkoa wa Njombe ambapo timu zingine ziliweza kushiriki na hatimae mwaka 2023 Michuano hii ziliingiza timu 16 na Mwaka huu timu 21 zimethibitisha kushiriki hivyo mtaona Mashindano yalivopata muamko mkubwa wakimichezo kwa vijana.”

Hata hivyo ameongeza kuwa wadhamini wanakaribishwa katika Mashindano hayo ili kuendelea kuwapa Moyo na hamasa Vijana wa Mikoani ambao wana vipaji vya michezo hasa soka.

Related Posts