MAFANIKIO YA TANROADS KWENYE UJENZI WA MIUNDOMBINU MKOANI KAGERA

Mafanikio hayo hii leo yanaangazia Wakala wa Barabara TANROADS Mkoani Kagera mkoa ambao unasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 1,966.29 ambapo Kati ya hizo barabara kuu ni Kilomita 861.59, barabara za mkoa ni kilomita 1,053.75 na barabara za wilaya ni kilomita 50.95.

Kama unavyofahamu licha ya TANROADS kusimamia matengenezo ya barabara na madaraja, katika kipindi cha miaka mitatu Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya Kimkakati ambayo utekelezaji wake upo kwenye hatua mbalimbali na jumla ya miradi hiyo inagharimu Tshs bilioni 431.474

 

Related Posts