Mustafa aaga El Merriekh, kuendelea kuwepo Ligi Kuu Bara

Kipa wa El Merriekh ya Sudan, Mohamed Mustafa aliyekuwa akikipiga Azam FC  hapo kwa mkopo, inaelezwa amepewa ofa ya kusaini mkataba wa miaka miwili na matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam.

Mustafa ameisaidia  kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024-25 baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho (FA).

Kipa huyo aliyejiunga na El Merriekh tangu akiwa na miaka sita, kwenye ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe wa kuaga timu hiyo na kuonyesha wazi ataendelea kukipiga Azam FC

“Sitauita utengano kwa sababu tofauti ni umbali, kiakili na kiroho, huku mimi niko mbali kimwili, haitawezekana kuondoa asili yangu, nyumba yangu na wale walionifanya kuwa hivi,” alisema kipa huyo na kuendelea;

“Sipo kutafuta tu changamoto na uzoefu tofauti, nitaendelea kuwa balozi mzuri wa klabu ya watu. Asante familia yangu iliyoniunga mkono na kuonyesha uvumilivu kwangu na kufanikiwa katika viwango vipya. Asante Rais wa klabu, Mhandisi Omar Al-Munbar, Asante Bw. Kambal Abdullah Kambal kwa kunipa fursa hii. Shukrani za kipekee kwa mashabiki wa timu hii kubwa ambayo ilinipa fursa ya kuwakilisha Mars na Sudan nje ya nchi. Natumai tutakutana tena siku zijazo.”

Kufanya vizuri kwa kipa huyo kulimfanya kocha wa kikosi hicho, Youssouph Dabo kupendekeza kusajiliwa jumla katika ripoti yake.

Hapo awali Mwanaspoti liliripoti Azam FC imevutiwa na huduma ya kipa huyo na iliandika maombi ya kuhitaji kumnunua moja kwa moja na Merriekh ilikataa na kueleza bado inauhitaji na mchezaji huyo.

Kuaga kwake kunaonyesha dhahiri kuwa nyota huyo ataendelea kuonekana Ligi Kuu Bara licha ya kuwa na ofa nyingine nyingi, kwani Mwanaspoti liliwahi kupiga stori na nyota huyo na aliweka wazi kutamani kuendelea kucheza Tanzania.

Related Posts